Matembezi ya Betheli
Tunakualika kwa uchangamfu utembelee ofisi zetu za tawi, tunazoziita Betheli. Baadhi ya ofisi zetu zina maonyesho utakayotembelea ukiwa peke yako.
Afrika Kusini
Habari Kuhusu Matembezi
Mambo yenye kupendeza
Kituo cha Wageni Katika Idara ya Makao. Utaona video ya utangulizi inayoonyesha mambo ambayo yanafanywa Betheli na pia utaelewa jinsi Betheli inavyotegemeza ibada yetu.
Kituo cha Wageni Katika Jengo la 2 la Uchapishaji. Utaona video inayoonyesha umuhimu wa kuchapisha machapisho yetu katika lugha mbalimbali. Kuna kibaraza kilicho juu kinachowawezesha wageni kuona mashine za uchapishaji zikifanya kazi. Maonyesho ya Biblia yanaonyesha historia ya jinsi Biblia za lugha mbalimbali za eneo hilo zimetumia jina la Mungu.
Kituo cha Wageni Katika Jengo la 3 la Uchapishaji. Kuna kibaraza kilicho juu kinachokuwezesha kuona eneo lote la upakiaji.
Habari za Ziada. Wageni wanaweza kufurahia kula chakula walichobeba katika Eneo la Kupumzikia Wageni.
Anwani na Namba ya Simu

