Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

 SEHEMU YA 3

Huduma Kuu ya Yesu Huko Galilaya

‘Yesu akaanza kuhubiri: “Ufalme umekaribia.”’​—Mathayo 4:17

Huduma Kuu ya Yesu Huko Galilaya

KATIKA SEHEMU HII

SURA YA 20

Muujiza wa Pili Huko Kana

Yesu amponya mtoto akiwa umbali wa kilomita 26.

SURA YA 21

Katika Sinagogi Huko Nazareti

Yesu alisema jambo gani ambalo lilifanya watu wa mji wa nyumbani kwao watake kumuua?

SURA YA 22

Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu

Anawaalika waache aina moja ya uvuvi na kuanza aina nyingine.

SURA YA 23

Yesu Afanya Miujiza Huko Kapernaumu

Yesu anapowafukuza roho waovu, anawakataza roho hao wasiwaambie watu kwamba yeye ndiye Mwana wa Mungu. Kwa nini?

SURA YA 24

Apanua Huduma Yake Huko Galilaya

Watu wanakuja kwa Yesu ili waponywe, lakini Yesu anaeleza kwamba huduma yake ina kusudi kubwa zaidi.

SURA YA 25

Amponya Mtu Mwenye Ukoma kwa Huruma

Kwa maneno rahisi lakini yenye nguvu, Yesu anathibitisha kwamba anawajali sana watu anaowaponya.

SURA YA 26

“Umesamehewa Dhambi Zako”

Yesu anaonyesha uhusiano gani uliopo kati ya dhambi na magonjwa?

SURA YA 27

Mathayo Aitwa

Kwa nini Yesu anafurahia kula mlo pamoja na watenda dhambi sugu?

SURA YA 28

Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?

Yesu anatumia mfano wa kiriba cha ngozi cha divai ili kujibu.

SURA YA 29

Je, Mtu Anaweza Kufanya Mambo Mema Siku ya Sabato?

Kwa nini Wayahudi wanamtesa Yesu kwa kuponya mtu aliyekuwa mgonjwa miaka 38?

SURA YA 30

Uhusiano Kati ya Yesu na Baba Yake

Wayahudi wanafikiri kwamba Yesu anajilinganisha na Mungu, lakini Yesu anaonyesha wazi kwamba Mungu ni mkuu kuliko yeye.

SURA YA 31

Wakata Masuke ya Nafaka Siku ya Sabato

Kwa nini Yesu anajiita “Bwana wa Sabato?”

SURA YA 32

Ni Mambo Gani Yaliyo Halali Siku ya Sabato?

Ingawa kwa kawaida Masadukayo na Mafarisayo hawaelewani, sasa wanaungana wakiwa na nia moja.

SURA YA 33

Atimiza Unabii wa Isaya

Kwa nini Yesu anaamuru wale anaowaponya wasiwaambie wengine yeye ni nani au mambo ambayo amefanya?

SURA YA 34

Yesu Achagua Mitume Kumi na Wawili

Kuna tofauti gani kati ya mwanafunzi na mtume?

SURA YA 35

Mahubiri Maarufu ya Mlimani

Pata ufafanuzi wa mambo makuu katika hotuba ya Yesu.

SURA YA 36

Imani Kubwa ya Ofisa wa Jeshi

Ofisa huyu wa jeshi anafanya jambo gani ambalo linamshangaza Yesu?

SURA YA 37

Yesu Amfufua Mwana wa Mjane

Wale walioona muujiza huu walielewa ulivyomaanisha kikweli.

SURA YA 38

Yohana Anataka Kusikia Kutoka kwa Yesu

Kwa nini Yohana Mbatizaji anauliza kama Yesu ndiye Masihi? Je, Yohana ana shaka?

SURA YA 39

Ole kwa Kizazi Kisichotii

Yesu anasema kwamba katika Siku ya Hukumu, itakuwa afadhali zaidi kwa nchi ya Sodoma kuliko kwa Kapernaumu, jiji ambalo amekaa kwa muda fulani.

SURA YA 40

Somo Kuhusu Msamaha

Yesu alipomwambia mwanamke ambaye huenda alikuwa kahaba amesamehewa dhambi zake, je, alikuwa akisema ni sawa kuvunja sheria ya Mungu?

SURA YA 41

Anafanya Miujiza kwa Nguvu za Nani?

Ndugu za Yesu wanaamini kwamba Yesu amerukwa na akili.

SURA YA 42

Yesu Awakemea Mafarisayo

“Ishara ya nabii Yona” ni nini?

SURA YA 43

Mifano Kuhusu Ufalme wa Mbinguni

Yesu anatoa mifano minane ili kuelezea mambo mbalimbali kuhusu Ufalme mbinguni.

SURA YA 44

Yesu Atuliza Dhoruba Baharini

Yesu anapotuliza upepo na mawimbi, anafundisha somo muhimu kuhusu maisha yatakavyokuwa chini ya Ufalme wake.

SURA YA 45

Ana Nguvu Kuliko Kikosi cha Roho Waovu

Je, mtu anaweza kuingiwa na roho wengi waovu?

SURA YA 46

Aponywa kwa Kugusa Vazi la Yesu

Yesu anaonyesha nguvu zake na huruma katika tukio linalogusa moyo.

SURA YA 47

Msichana Mdogo Afufuliwa!

Watu wanamcheka Yesu anaposema kwamba msichana aliyekufa amelala tu. Ni nini anachojua ambacho hawajui?

SURA YA 48

Afanya Miujiza, Lakini Akataliwa Hata Huko Nazareti

Watu wa Nazareti hawamkatai Yesu kwa sababu ya mafundisho yake au miujiza yake, bali wana sababu nyingine.

SURA YA 49

Kuhubiri Galilaya na Kuwazoeza Mitume

Maneno “Ufalme wa mbinguni umekaribia” yanamaanisha nini hasa?

SURA YA 50

Tayari Kuhubiri Licha ya Mateso

Kwa nini Yesu anawaambia wakimbie wanapoteswa, ilhali hawapaswi kuogopa kifo?

SURA YA 51

Mauaji Kwenye Sherehe ya Sikukuu ya Kuzaliwa

Herode anafurahishwa sana na jinsi Salome anavyocheza dansi hivi kwamba anaahidi kumpa chochote atakachoomba. Anaomba jambo gani la ukatili?

SURA YA 52

Alisha Maelfu kwa Mikate na Samaki Wachache

Muujiza wa Yesu ni muhimu sana hivi kwamba vitabu vyote vinne vya Injili vinautaja.

SURA YA 53

Mtawala Anayeweza Kudhibiti Nguvu za Asili

Wanafunzi wanajifunza somo gani Yesu anapotembea juu ya maji na kuutuliza upepo?

SURA YA 54

Yesu​—“Mkate Kutoka Mbinguni”

Kwa nini Yesu anawakemea watu ingawa walijitahidi sana kumtafuta?

SURA YA 55

Maneno ya Yesu Yawashtua Wengi

Yesu anafundisha jambo lenye kushtua sana hivi kwamba wengi kati ya wanafunzi wake wanaacha kumfuata.

SURA YA 56

Ni Nini Hasa Kinachomchafua Mtu?

Je, ni kile kinachoingia mdomoni, au kile kinachotoka mdomoni?

SURA YA 57

Yesu Amponya Msichana na Mwanamume Kiziwi

Kwa nini mwanamke fulani hakasiriki Yesu anapolinganisha watu wa taifa lake na mbwa wadogo?

SURA YA 58

Afanya Mikate Iongezeke Kimuujiza na Kuonya Kuhusu Chachu

Mwishowe wanafunzi wa Yesu wanaelewa kuhusu aina ya chachu ambayo anazungumzia.

SURA YA 59

Mwana wa Binadamu Ni Nani?

Funguo za Ufalme ni zipi? Ni nani anayezitumia, na jinsi gani?

SURA YA 60

Kugeuka Sura​—Wamwona Kristo Katika Utukufu

Kugeuka sura ni nini? Kulimaanisha nini?

SURA YA 61

Yesu Amponya Mvulana Mwenye Roho Mwovu

Yesu anasema kwamba walishindwa kumponya kwa kukosa imani, lakini kwa nani? Mvulana, baba yake, au wanafunzi wake?

SURA YA 62

Somo Muhimu Kuhusu Unyenyekevu

Watu wazima wanajifunza jambo muhimu kutoka kwa mtoto mdogo.

SURA YA 63

Yesu Atoa Ushauri Kuhusu Kukwaza na Dhambi

Anafafanua hatua tatu za kushughulikia mambo mazito kati ya ndugu.

SURA YA 64

Umuhimu wa Kusamehe

Yesu anatumia mfano wa mtumwa asiye na rehema kuonyesha kwamba Mungu anaona utayari wetu wa kuwasamehe wengine kuwa jambo zito.

SURA YA 65

Kufundisha Akiwa Safarini Kwenda Yerusalemu

Yesu anazungumza na watu watatu na kuonyesha mitazamo inayoweza kumzuia mtu kumfuata.