Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mambo Makuu ya Sehemu ya 2

Mambo Makuu ya Sehemu ya 2

Zungumzia maswali yafuatayo pamoja na mwalimu wako:

  1. Mungu atachukua hatua gani dhidi ya dini za uwongo?

    (Ona Somo la 13.)

  2. Soma Kutoka 20:4-6.

    • Yehova anahisije watu wanapodai kwamba wanamwabudu kwa kutumia sanamu?

      (Ona Somo la 14.)

  3. Yesu ni nani?

    (Ona Somo la 15.)

  4. Unapenda sifa gani za Yesu?

    (Ona Somo la 17.)

  5. Soma Yohana 13:34, 35 na Matendo 5:42.

    • Ni nani wanaotenda kupatana na Ukristo wa kweli leo? Ni nini kinachokuthibitishia kwamba wao ni Wakristo wa kweli?

      (Ona Somo la 18 na la 19.)

  6. Kichwa cha kutaniko ni nani, naye anaongozaje kutaniko?

    (Ona Somo la 20.)

  7. Soma Mathayo 24:14.

    • Unabii huu unatimizwaje leo?

    • Umezungumza na nani kuhusu habari njema?

      (Ona Somo la 21 na la 22.)

  8. Je, unafikiri kwamba ubatizo ni lengo muhimu? Kwa nini?

    (Ona Somo la 23.)

  9. Unaweza kujilindaje dhidi ya Shetani na roho waovu?

    (Ona Somo la 24.)

  10. Kusudi la Mungu kwa wanadamu ni nini?

    (Ona Somo la 25.)

  11. Kwa nini wanadamu huteseka na kufa?

    (Ona Somo la 26.)

  12. Soma Yohana 3:16.

    • Yehova amefanya nini ili kutuokoa kutoka katika dhambi na kifo?

      (Ona Somo la 27.)

  13. Soma Mhubiri 9:5.

    • Ni nini hutokea mtu anapokufa?

    • Yesu atafanya nini kuhusu mabilioni ya watu waliokufa?

      (Ona Somo la 29 na la 30.)

  14. Kwa nini Ufalme wa Mungu ni bora kuliko serikali nyingine zote?

    (Ona Somo la 31 na la 33.)

  15. Je, unaamini kwamba Ufalme wa Mungu unatawala? Kwa nini? Ufalme huo ulianza kutawala lini?

    (Ona Somo la 32.)