Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Hadithi ya 90: Pamoja na Mwanamke Penye Kisima

Hadithi ya 90: Pamoja na Mwanamke Penye Kisima

YESU amekaa akipumzika karibu na kisima Samaria. Wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. Mwanamke anayesema na Yesu amekuja kuteka maji. Yesu amwambia: ‘Nipe maji ninywe.’

Yesu akizungumza na mwanamke Msamaria

Mwanamke anashangaa sana kusikia hivyo. Unajua sababu? Yesu ni Myahudi, na mwanamke ni Msamaria. Na Wayahudi wengi hawapendi Wasamaria. Hawataki hata kusema nao! Lakini Yesu anapenda watu wa namna zote. Amwambia mwanamke hivi: ‘Wewe ukimjua anayekuomba maji, ungemwomba akupe maji yanayotoa uzima.’

‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘kisima ni kirefu, na huna ndoo. Utapata wapi maji hayo yanayotoa uzima?’

‘Ukinywa maji ya kisima hiki utaona kiu tena,’ Yesu amweleza. ‘Lakini maji nitakayotoa yanaweza kumfanya mtu aishi milele.’

‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘nipe maji hayo! Nisione kiu tena. Nisije tena huku kuteka maji.’

Mwanamke huyo anadhani Yesu anasema maji halisi. Lakini anasema juu ya kweli ya Mungu na ufalme wake. Kweli hiyo ni kama maji yanayotoa uzima. Inaweza kumpa mtu uzima wa milele.

Sasa Yesu anamwambia mwanamke hivi: ‘Nenda kamwite mume wako urudi.’

‘Sina mume,’ anajibu.

‘Umejibu sawa,’ Yesu asema. ‘Lakini umekuwa na waume watano, na yule uliye naye sasa si mume wako.’

Yule mwanamke astaajabu, kwa sababu yote hayo ni kweli. Yesu alijuaje hayo? Ni kwa vile Yesu Ndiye aliyeahidiwa akatumwa na Mungu, naye Mungu anamjulisha hayo. Wakati huo wanafunzi wa Yesu wanarudi, nao wanashangaa kumwona akizungumza na mwanamke Msamaria.

Twajifunza nini kwa hayo? Kwamba Yesu anapenda wat wa mataifa yote. Sisi pia tuwa hivyo. Tusidhani watu wengine ni wabaya kwa sababu ni wa taifa fulani. Yesu anataka watu wote waijue kweli inayoongoza kwenye uzima. Na sisi pia yatupasa tuwe na nia ya kusaidia watu wajifunze kweli.

Yohana 4:5-43; 17:3.Maswali

  • Kwa nini Yesu ametua kwenye kisima huko Samaria, na anamwambia mwanamke mmoja nini?
  • Kwa nini mwanamke huyo anashangaa, Yesu anamwambia nini, na kwa nini?
  • Mwanamke huyo anafikiri Yesu anaongea kuhusu maji ya aina gani, lakini Yesu anaongea juu ya maji gani?
  • Kwa nini mwanamke huyo anashangaa kusikia kwamba Yesu anajua mambo mengi kumhusu, na Yesu anajuaje mambo hayo?
  • Tunaweza kujifunza nini kutokana na masimulizi kumhusu mwanamke huyo kwenye kisima?

Maswali ya ziada