Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Sehemu 5: Utumwa Babeli Mpaka Kujengwa Upya Kuta za Yeruslamu

Sehemu 5: Utumwa Babeli Mpaka Kujengwa Upya Kuta za Yeruslamu

Wakiwa utumwani Babeli, imani ya Waisraeli ilijaribiwa sana. Shadraka, Meshaki na Abed′ne·go walitupwa katika tanuru (jiko) ya moto mkali, lakini Mungu akawaokoa. Baadaye, Babeli ukiisha kushindwa na Wamedi na Waajemi, Danieli alitupwa katika shimo la simba, lakini Mungu alimlinda pia kwa kuvifunga vinywa vya simba.

Mwishowe, Koreshi mfalme wa Ajemi akawakomboa Waisraeli. Walirudi kwao ilipotimia miaka 70 baada ya kupelekwa Babeli kama mateka. Jambo la kwanza walilofanya waliporudi Yerusalemu ni kujenga hekalu la Yehova. Lakini, upesi adui wakazuia kazi yao. Hivyo walimaliza kujenga hekalu kwa muda wa karibu miaka 22 baada ya kurudi Yerusalemu.

Halafu, tunajifunza habari ya safari ya Ezra akirudi Yerusalemu akalipambe hekalu. Hiyo ilikuwa miaka 47 baada ya kumaliza kujenga hekalu. Kisha, miaka 13 baada ya safari ya Ezra, Nehemia alisaidia kujenga upya kuta za Yerusalemu zilizobomoka. Sehemu ya 5 inazungumza historia ya miaka 152 kufikia wakati huo.

Ezra pamoja na watu wakisali