Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Hadithi ya 72: Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia

Hadithi ya 72: Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia

UNAJUA sababu mwanamume huyu anamwomba Yehova? Kwa nini ameweka barua hizi mbele ya madhabahu ya Yehova? Mwanamume huyu ni Hezekia. Ni mfalme wa makabila mawili ya kusini ya Israeli. Ana taabu nyingi. Kwa nini?

Mfalme Hezekia akisali

Kwa sababu majeshi ya Ashuru yamekwisha haribu makabila 10 ya kaskazini. Yehova aliruhusu hayo yatokee kwa sababu watu hao walikuwa wabaya sana. Na sasa majeshi ya Ashuru yamekuja kupigana na ufalme wa makabila mawili.

Mfalme wa Ashuru amempelekea Mfalme Hezekia barua sasa hivi. Hizo ndizo barua ambazo Hezekia ameweka mbele za Mungu. Ni barua za kumcheka Yehova, na kumwambia Hezekia akubali kushindwa. Ndiyo sababu Hezekia anaomba hivi: ‘Ee Yehova, utuokoe na mfalme wa Ashuru. Ndipo mataifa yote yatakapojua wewe peke yako ndiwe Mungu.’ Yehova atamsikiliza Hezekia?

Hezekia ni mfalme mzuri. Yeye si kama wafalme wale wabaya wa ufalme wa Israeli wa makabila 10, wala si kama baba yake Ahazi, mfalme mbaya. Hezekia ametii sana sheria zote za Yehova. Basi, Hezekia akiisha kusali, nabii Isaya anampelekea ujumbe huu wa Yehova: ‘Mfalme wa Ashuru hataingia Yerusalemu. Askari zake hawataukaribia. Hawataupiga mji huo hata mshale mmoja.’

Itazame picha ya ukurasa huu. Unajua ni askari gani hawa wote waliokufa? Ni Waashuru. Yehova alimtuma malaika wake, na usiku mmoja malaika huyo akaua askari wa Ashuru 185,000. Lakini baada ya Hezekia kufa Manase mwanawe anakuwa mfalme. Manase na Amoni mwanawe anayemfuata ni wafalme wabaya sana. Hivyo nchi tena yajaa uhalifu na jeuri. Mfalme Amoni anapouawa na watumishi wake, Yosia mwanawe anafanywa mfalme wa ufalme wa makabila mawili.

Askari Waashuru waliokufa

2 Wafalme 18:1-36; 19:1-37; 21:1-25.



Maswali

  • Mtu unayemwona katika picha ni nani, na kwa nini yuko tabaani?
  • Ni barua gani ambazo Hezekia ameweka mbele za Mungu, na Hezekia anamwomba Yehova nini?
  • Je, Hezekia ni mfalme mzuri au mbaya, na Yehova anamtuma Isaya ampelekee ujumbe gani?
  • Kama picha inavyoonyesha, malaika wa Yehova anawafanya Waashuru nini?
  • Ijapokuwa ufalme wa makabila mawili una amani kwa muda, ni nini kinachotokea baada ya kifo cha Hezekia?

Maswali ya ziada