Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Sehemu 4: Mfalme wa Kwanza wa Israeli Mpaka Utumwa Babeli

Sehemu 4: Mfalme wa Kwanza wa Israeli Mpaka Utumwa Babeli

Sauli (Saulo) akawa mfalme wa kwanza wa Israeli. Lakini Yehova alimkataa, Daudi akachaguliwa awe mfalme badala yake. Tunajifunza mambo mengi juu ya Daudi. Akiwa kijana, alipigana na jitu Goliathi. Baadaye alimkimbia Mfalme Sauli mwenye wivu. Kisha Abigaili mwenye sura nzuri akamzuia asitende upumbavu.

Halafu, tunajifunza mengi juu ya Sulemani (Solomono), mwana wa Daudi, aliyechukua mahali pa Daudi awe mfalme wa Israeli. Kila mmoja wa wafalme watatu wa kwanza wa Israeli alitawala kwa miaka 40. Baada ya Sulemani kufa, Israeli waligawanyika kuwa falme mbili, ufalme wa kaskazini na wa kusini.

Ufalme wa kaskazini wa makabila 10 uliendelea muda wa miaka 257 kabla ya kuharibiwa na Waashuru. Halafu miaka 133 baadaye, ufalme wa kusini wa makabila mbili ukaharibiwa pia. Wakati huu Waisraeli walihamishwa kupelekwa Babeli. Hivyo Sehemu ya 4 inazungumza historia ya miaka 510, muda ambao mambo mengi ya kusisimua yanatukia mbele yetu.

Mfalme Sulemani akiomba