Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Hadithi ya 20: Dina Anaingia Katika Taabu

Hadithi ya 20: Dina Anaingia Katika Taabu

UNAONA Dina anaenda kutembela nani? Ni wasichana wanaokaa Kanaani. Je! Yakobo baba yake atafurahia? Ili uweze kujibu ulizo hilo, jaribu kukumbuka Ibrahimu na Isaka walivyofikiria wanawake wa Kanaani.

Dina akiwatembelea wasichana wa Kanaani

Je! Ibrahimu alitaka Isaka aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Je! Isaka na Rebeka walitaka Yakobo aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Unajua sababu yake?

Ni kwa sababu watu hao wa Kanaani waliabudu miungu ya uongo. Hawakufaa kuwa waume na wake, nao hawakufaa kuwa rafiki wa kushirikiana nao. Basi tunaweza kuwa na hakika kwamba Yakobo hangependezwa na urafiki wa binti yake pamoja na wasichana hao Wakanaani.

Bila shaka, Dina aliingia katika taabu. Je! unamwona mwanamume huyo Mkanaani katika picha anayemtazama Dina? Ni Shekemu. Siku moja Dian alipokuwa akitembelea, Shekemu alimchukua na kumlazimisha alale naye. Hilo lilikuwa kosa, kwa sababu ni wanaume na wanawake waliooana tu ndio wanaotakiwa kulala pamoja. Ubaya huo ambao Shekemu alimtendea Dina uliongoza kwenye taabu nyingi zaidi.

Ndugu zake Dina waliposikia yaliyotokea, walikasirika sana. Simeoni na Levi, walikasirika sana hata wakachukua panga wakaingia mjini na kuwafikia wanaume hao ghafula. Wao na ndugu zao wakamwua Shekemu na wanaume wengine wote. Yakobo alikasirika kwa sababu wanawe walifanya ubaya huo.

Taabu yote hiyo ilianza namna gani? Ni kwa sababu Dina alifanya urafiki na watu ambao hawakutii sheria za Mungu. Hatutaki tufanye urafiki na watu kama hao, sivyo?

Mwanzo 34:1-31.Maswali

  • Kwa nini Ibrahimu na Isaka hawakutaka watoto wao waoe au waolewe na Wakanaani?
  • Je, Yakobo alifurahia kwamba binti yake alifanya urafiki na wasichana Wakanaani?
  • Yule mtu anayemtazama Dina katika picha ni nani, na alifanya tendo gani baya sana?
  • Ndugu za Dina, Simeoni na Lawi, walifanya nini waliposikia jambo hilo?
  • Yakobo alikubali walichofanya Simeoni na Lawi?
  • Matatizo yote ya familia yao yalianzaje?

Maswali ya ziada