Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Yesu akizungumza na watoto

HIKI ni kitabu cha hadithi za kweli. Zimetolewa katika Biblia kitabu kikubwa zaidi ulimwenguni. Hadithi hizo zinakupa historia ya ulimwengu kutoka Mungu alipoanza kuumba vitu mpaka leo. Zinasimulia hata yale ambayo Mungu anaahidi kufanya wakati ujao.

Kitabu hiki kinakufahamisha Biblia. Kinasimulia habari za watu wanaotajwa katika Biblia na mambo waliyofanya. Kinaonyesha pia tumaini bora ambalo Mungu amewapa watu juu ya uzima wa milele katika dunia iliyo paradiso.

Kitabu hiki kina hadithi 116. Nazo zimepangwa katika sehemu nane. Ukurasa mwanzoni mwa kila sehemu unasimulia kifupi yanayopatikana katika sehemu hiyo. Hadithi hizo zinasimuliwa kufuatana na namna mambo yalivyotokea katika historia. Hiyo inakusaidia ujue wakati mambo yalipotokea katika historia, kuhusiana na mengine.

Hadithi hizo zimesimuliwa kwa Kiswahili rahisi. Wengi kati yenu ninyi watoto wataweza kujisomea wenyewe. Ninyi wazazi mtaona kwamba watoto wenu wachange watafurahi kusomewa hadithi hizo mara nyingi. Mtaona kitabu hiki kina mengi ya kupendeza watoto na wakubwa.

Mitajo ya Biblia imetolewa mwishoni mwa kila hadithi. Mnatiwa moyo kusoma sehemu hizo za Biblia iliyo msingi wa hadithi hizi.

Maneno ya Biblia yamesimuliwa kifupi katika kitabu hiki. Yameandikwa kwa Kiswahili rahisi ili watoto wachanga waweze kuyafahamu. Mitajo iliyo mwishoni mwa kila hadithi imetokana na Biblia.