Tunakuthamini, Dada Mpendwa
Pakua:
1. Wewe dada yangu mwenye thamani
Ninachochewa na imani uliyo nayo.
Ninavutiwa na kazi zako
Imefanya nikuimbie wimbo huu.
(KIBWAGIZO)
Unapochoka maneno ya wimbo,
Yakufariji.
(KORASI)
Dada mpendwa,
Twaona bidii yako.
Watabasamu
Licha ya magumu yako.
Laiti ungejiona mwenyewe,
Basi ungejua kwamba.
Twakuthamini.
2. Usaidiapo wewe hujigambi
Licha ya mengi unayofanya kwa wengine.
Ukitoa Zawadi hujisifu.
Unachochea wengine wawe wa’minifu.
(KIBWAGIZO)
Usifikiri Imani yako bure
Yatuchochea.
(KORASI)
Dada mpendwa,
Twaona bidii yako.
Watabasamu
Licha ya magumu yako.
Laiti ungejiona mwenyewe,
Basi ungejua kwamba.
Twakuthamini.
(DARAJA)
Yehova anakuona.
Anajua wewe ni wa thamani
Watumikia wengine.
(KORASI)
Dada mpendwa,
Twaona bidii yako.
Watabasamu
Licha ya magumu yako.
Laiti ungejiona mwenyewe,
Basi ungejua kwamba.
Twakuthamini.
(MWISHO)
Twataka uwe na shangwe.
Yehova hatasahau.
Dada Mpendwa.
Mpendwa, Tunakuthamini.
Twakuthamini.

