WIMBO NA. 57
Kuwahubiria Watu wa Namna Zote
-
1. Twatamani kumwiga Yehova,
Mungu asiye na ubaguzi.
Ni mapenzi yake watu wote,
Wapate uzima wa milele.
(KORASI)
Hatutazami sura;
Wala hali za watu.
Twatangazia wote ujumbe.
Kwa kuwa twawajali,
Twawakaribisha wote,
Wawe rafiki za Yehova.
-
2. Haidhuru wapatikanapo,
Wanavyoonekana mwanzoni.
La muhimu, walivyo moyoni—
Alivyo yule mtu wa ndani.
(KORASI)
Hatutazami sura;
Wala hali za watu.
Twatangazia wote ujumbe.
Kwa kuwa twawajali,
Twawakaribisha wote,
Wawe rafiki za Yehova.
-
3. Yehova awapa wote fursa,
Waache njia za ulimwengu.
Tuna hamu kujulisha wengi,
Basi tuwahubirie wote.
(KORASI)
Hatutazami sura;
Wala hali za watu.
Twatangazia wote ujumbe.
Kwa kuwa twawajali,
Twawakaribisha wote,
Wawe rafiki za Yehova.
(Ona pia Yoh. 12:32; Mdo. 10:34; 1 Tim. 4:10; Tit. 2:11.)

