WIMBO NA. 119
Lazima Tuwe na Imani
-
1. Kale Yehova Mungu kasema,
Kupitia manabii.
Leo kupitia Mwana wake,
Anasema: ‘Tubuni! ’
(KORASI)
Je, tuna imani kweli?
Ni lazima tuijenge.
Je, ni ya matendo kweli?
Imani iokoayo nafsi.
-
2. Amri ya Yesu Kristo twatii,
Ufalme tunatangaza.
Tuutangaze ujumbe wake
Utakaotimizwa.
(KORASI)
Je, tuna imani kweli?
Ni lazima tuijenge.
Je, ni ya matendo kweli?
Imani iokoayo nafsi.
-
3. Tuna imani nayo ni ngao;
Kamwe hatutaogopa.
Tunavumilia tukijua,
Wokovu u karibu.
(KORASI)
Je, tuna imani kweli?
Ni lazima tuijenge.
Je, ni ya matendo kweli?
Imani iokoayo nafsi.
(Ona pia Rom. 10:10; Efe. 3:12; Ebr. 11:6; 1 Yoh. 5:4.)

