Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kwa Ajili Ya Vijana

Epuka Kujitakia Makuu!

Epuka Kujitakia Makuu!

Maagizo: Fanya zoezi hili katika mazingira matulivu. Unaposoma maandiko, jiwazie ukiwa katika matukio yanayozungumziwa. Wazia kikao. Sikia sauti. Hisi kama wahusika wanavyohisi. Wazia kwamba masimulizi haya ni halisi kabisa.

Wahusika wakuu: Daudi, Absalomu, Yoabu

Muhtasari: Absalomu ajaribu kupindua ufalme wa baba yake.

CHUNGUZA TUKIO HILI.—SOMA 2 SAMWELI 14:25-33; 15:1-17; 18:9-17, 30-33.

Eleza jinsi Absalomu alivyoonekana, kama unavyomwazia. (Soma tena 2 Samweli 14:25, 26.)

Unawazia sauti na mtazamo wa Absalomu ulikuwaje alipokuwa akishawishi mioyo ya watu waliokuja kwa mfalme kutafuta haki? (Soma tena 2 Samweli 15:2-6.)

Unatambua nini kuhusu utu wa Absalomu kutokana na tukio lililoandikwa kwenye 2 Samweli 14:28-30?

CHIMBA ZAIDI.

Absalomu alikuwa amefanya mpango gani ili kunyakua ufalme? (Dokezo: Soma 2 Samweli 13:28, 29. Amnoni alikuwa mwana mzaliwa wa kwanza wa Daudi na hivyo angerithi kiti cha ufalme.)

Ingawa alikuwa na tamaa ya kupata makuu na alijaribu kujitafutia sifa, jinsi Absalomu alivyozikwa inaonyesha nini kuhusu vile ambavyo kwa kweli watu walimwona?(Soma tena 2 Samweli 18:17.)

Unafikiri ni nini kilichochangia Absalomu awe na roho ya kujitakia makuu? (Kwa kulinganisha, soma maelezo kuhusu Diotrefe kwenye 3 Yohana 9, 10.)

Daudi aliathiriwaje na matendo ya Absalomu? (Dokezo: Soma Zaburi ya 3, ambayo Daudi aliiandika wakati wa uasi wa Absalomu.)

TUMIA MAMBO ULIYOJIFUNZA. ANDIKA MAMBO ULIYOJIFUNZA KUHUSU  . . .

Hatari ya kujitakia makuu.

Maumivu ambayo mtu anaweza kuwasababishia wengine, kutia ndani wazazi wake, kwa sababu ya matendo yake.

NJIA NYINGINE UNAYOWEZA KUTUMIA HABARI HIYO.

Unawezaje kunaswa na mtego wa kujitakia makuu?

Unawezaje kuepuka kusitawisha kiburi?

NI MAMBO GANI KATIKA SIMULIZI HILI AMBAYO YAMEKUGUSA MOYO SANA, NA KWA NINI?

Mapendekezo: Wazia matokeo yangekuwaje ikiwa Absalomu angetenda ifaavyo. Ni nini ambacho kingetokea ikiwa Absalomu angekuwa mwenye kiasi badala ya kujitakia makuu?—Methali 18:12.