Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Karne ya 20 Ilitawaliwa na Shetani?

Je, Karne ya 20 Ilitawaliwa na Shetani?

Je, Karne ya 20 Ilitawaliwa na Shetani?

“KARNE ya 20 inafaa kuitwa karne ya Shetani kwa kuzingatia uovu mwingi ambao umekuwako katika karne hiyo. Karne ya 20 imekuwa tofauti na karne zile nyingine kwa kuwa wanadamu wamekuwa na mwelekeo na tamaa ya kuua mamilioni ya wanadamu wenzao kwa sababu za kijamii, kidini au kiuchumi.”

Taarifa hiyo ilikuwa katika tahariri ya gazeti The New York Times la Januari 26, 1995 lililochapishwa wakati wa kuadhimisha miaka 50 tangu kukombolewa kwa wafungwa wasio na hatia waliokuwa kwenye kambi za kifo za Nazi. Wayahudi wapatao milioni sita waliuawa wakati wa yale Maangamizi Makubwa yanayojulikana sana katika historia. Raia wa Poland wapatao milioni tatu ambao si Wayahudi waliuawa katika yale yanayoitwa “Maangamizi Yaliyosahaulika.”

“Inakadiriwa kwamba kati ya mwaka wa 1900 hadi 1989 watu milioni 86 waliuawa wakati wa vita,” asema Jonathan Glover katika kitabu chake Humanity—A Moral History of the Twentieth Century. Aongeza kusema: “Watu chungu nzima wamekufa wakati wa vita katika karne ya ishirini. Haiwezekani kutaja hesabu sahihi ya watu waliokufa, kwa kuwa karibu asilimia sitini na saba (watu milioni 58) waliuawa katika vita viwili vya ulimwengu. Lakini iwapo watu wote waliokufa katika karne ya ishirini wangekufa kwa kufuatana, watu 2,500 wangekuwa wakifa vitani kila siku, yaani zaidi ya watu 100 kwa saa, kwa muda wa miaka tisini mfululizo.”

Hivyo, karne ya 20 ndiyo imekuwa na mauaji mengi zaidi katika historia ya wanadamu. Katika kichapo Hope Against Hope, Nadezhda Mandelstam aandika hivi: “Tumeona uovu ukienea baada ya viwango vya kibinadamu kudharauliwa na kuvunjwa.” Katika vita ya wema na uovu, je, kweli uovu umeshinda?

[Picha katika ukurasa wa 2 zimeandaliwa na]

COVER: Mother and daughter: J.R. Ripper/SocialPhotos

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

U.S. Department of Energy photograph