Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 6, 2001

Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 6, 2001

Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 6, 2001

MKUTANO WA KILA MWAKA wa washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania utafanywa Oktoba 6, 2001, kwenye Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, 2932 Kennedy Boulevard, Jersey City, New Jersey. Mkutano unaotangulia wa washiriki peke yao utafanywa saa 3:15 asubuhi, ukifuatwa na ule mkutano mkuu wa kila mwaka saa 4:00 asubuhi.

Washiriki wa shirika hilo wanapaswa kuijulisha Ofisi ya Mwandishi sasa juu ya badiliko lolote la anwani zao lililotokea mwaka uliopita ili zile barua za kawaida zenye taarifa na hati za kuwakilisha ziweze kuwafikia mwezi wa Julai.

Hati za uwakilishi, zitakazopelekewa washiriki pamoja na taarifa ya mkutano wa kila mwaka, zinapasa kurudishwa ili ziifikie Ofisi ya Mwandishi wa Sosaiti kabla ya Agosti 1. Inampasa kila mshiriki ajaze mambo yote yaliyo katika hati yake ya kumwakilisha na kuirudisha upesi, akieleza kama yeye mwenyewe atahudhuria mkutano au la. Habari zinazojazwa katika kila hati ya uwakilishi zinapaswa kutaja waziwazi jambo hilo, kwa kuwa ndizo zitakazotumiwa kubainisha ni nani watakaohudhuria.

Inatarajiwa kwamba kipindi chote cha mkutano, kutia ndani ule mkutano rasmi na ripoti mbalimbali, kitamalizika mwendo wa saa 7:00 alasiri. Hakutakuwa na kipindi cha alasiri. Kwa sababu nafasi ni ndogo, wale wenye tikiti tu ndio watakaoweza kuingia kwenye mkutano. Hakutakuwa na mpango wa kuunganisha majumba mengine kwa simu ili kuusikiliza mkutano huu wa kila mwaka.