Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mazungumzo ya Familia

Mazungumzo ya Familia

Patanisha Picha na Maandishi

Soma Mwanzo 1:1-31. Chora mstari kuunganisha kila picha na mstari wa Biblia unaopatana nao.(Picha hazijapangwa kwa mpangilio unaofaa.)

ZUNGUMZIENI PAMOJA:

 

Tunajuaje kwamba siku za uumbaji hazikuwa siku zenye urefu wa saa 24? DOKEZO:

DOKEZO: Soma Mwanzo 2:4; Zaburi 90:4.

Unajifunza nini kumhusu Yehova kutokana na kazi zake za uumbaji? DOKEZO: Soma

DOKEZO: Zaburi 115:16; Waroma 1:20; 1 Yohana 4:8; Ufunuo 4:11.

UTENDAJI WA FAMILIA:

 

Pangeni kutembelea mahali fulani mkiwa familia. Tembeleeni bustani ya wanyama, bustani, au jengo lenye mitambo ya kuigiza miendo ya sayari, ili kujifunza mambo mengi kuhusu wanyama mnaopenda, mimea, au hata sayari. Kisha, zungumzeni mkiwa familia mambo ambayo mmejifunza kumhusu Yehova kwa kuchunguza uumbaji wake.

 Kusanya na Ujifunze

KADI YA BIBLIA 23 YONATHANI

MASWALI

 1. A. A. Yonathani alikuwa mwana mkubwa wa․․․․․.

 2. B. Kweli au Si kwali? Yonathani alirushiwa mkuki na baba yake.

 3. C. Yonathani alimpenda nani sana, na kwa nini?

MAMBO MACHACHE KUMHUSU

Ingawa alikuwa mrithi wa kiti cha ufalme na alimzidi Daudi kwa umri wa miaka 30 hivi, Yonathani alimuunga mkono Daudi ambaye alikuwa amechaguliwa na Mungu kuwa mfalme. (1 Samweli 23:15-18) Yonathani hata alihatarisha uhai wake ili kumlinda Daudi kutoka mikononi mwa Sauli, baba yake mwenye wivu. (1 Samweli 20:1-42) Mfano wa Yonathani wa unyenyekevu unatufundisha kuwa na furaha wengine wanapopata vitu vizuri kutoka kwa Mungu.

MAJIBU

 1. A. Mfalme Sauli.—1 Samweli 14:47, 49.

 2. B. Kweli.—1 Samweli 20:33.

 3. C. Daudi. Kwa sababu aliona ujasiri na upendo wa Daudi kwa Yehova wakati alipopambana na Goliathi.—1 Samweli 17:1–18:4.

Watu na Nchi

Majina yetu ni Pyae Sone Aung na Hsu Myat Yadanar Lwin. Nina umri wa miaka 11, na Hsu Myat Yadanar Lwin ana umri wa miaka 7. Tunaishi nchini Myanmar. Kuna Mashahidi wa Yehova wangapi nchini Myanmar? Je, ni 3,600, 6,300, au 10,000?

Ni alama gani inayoonyesha eneo tunaloishi? Chora duara kuizunguka na utie alama kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Myanmar.

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.

 MAJIBU

 1. 1 inapatana F.

 2. 2 inapatana B.

 3. 3 inapatana A.

 4. 4 inapatana E.

 5. 5 inapatana C.

 6. 6 inapatana D.

 7. 3,600.

 8. D.