Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Njia ya 2—Tunza Mwili Wako

Njia ya 2—Tunza Mwili Wako

 Njia ya 2—Tunza Mwili Wako

“Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake kwa vyovyote; bali huulisha na kuutunza.” (Waefeso 5:29) Kuchukua hatua rahisi kutunza mwili wako kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika afya yako.

◯ Pumzika vya kutosha. “Konzi moja ya pumziko ni afadhali kuliko konzi mbili za kazi ngumu na kufuatilia upepo.” (Mhubiri 4:6) Vikengeusha-fikira na hekaheka za maisha ya sasa zimefanya watu wasiwe na wakati wa kulala. Lakini usingizi ni muhimu ili mtu awe na afya nzuri. Utafiti umeonyesha kwamba tunapolala, mwili na ubongo wetu hujirekebisha, na hivyo kuboresha kumbukumbu na hisia zetu.

Usingizi huimarisha mfumo wa kinga na kupunguza hatari ya kupatwa na maambukizo, kisukari, ugonjwa wa moyo, kansa, kunenepa kupita kiasi, kushuka moyo, na pengine hata ugonjwa wa Alzheimer. Badala ya kuzuia usingizi kwa kula peremende, kafeini, au vitu vingine, tunapohisi usingizi tunapaswa kulala. Watu wazima wanahitaji kulala kwa kati ya saa saba au nane kila usiku ili wahisi na kuonekana wakiwa na afya na kufanya kazi vizuri. Vijana wanahitaji kulala kwa saa nyingi zaidi. Vijana ambao hawalali vyakutosha wanaweza kupatwa na matatizo ya kiakili na kusinzia wanapoendesha gari.

Usingizi ni muhimu hasa tunapokuwa wagonjwa. Miili yetu inaweza kushinda magonjwa fulani kama vile mafua tukilala kwa muda mrefu zaidi na kunywa vinywaji vingi.

◯ Tunza meno yako. Kupiga mswaki na kutumia uzi mwembamba kuondoa uchafu katikati ya meno kila baada ya kula, na hasa kabla ya kulala, kutazuia meno yasioze, magonjwa ya fizi, na kung’olewa jino. Bila meno hatuwezi kunufaika kabisa na vyakula tunavyokula. Inaripotiwa kwamba tembo hawafi kwa sababu ya uzee bali wao hufa polepole kwa sababu ya njaa kwa kuwa meno yao yanapodhoofika, wao hushindwa kutafuna chakula vizuri. Watoto ambao wamefundishwa kupiga mswaki na kuondoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi mwembamba baada ya kula watafurahia afya bora ujanani na maishani.

◯ Mwone daktari. Magonjwa fulani huhitaji uchunguzi wa daktari. Kwa kawaida, ugonjwa ukigunduliwa mapema, unaweza kutibiwa kwa urahisi na mtu atatumia pesa kidogo. Kwa hiyo, usipojihisi vizuri, badala ya kujaribu kutibu dalili tu, mwone daktari ili achunguze kisababishi ni nini.

Kufanyiwa uchunguzi kwa ukawaida na daktari anayeaminika kunaweza kuzuia matatizo mengine hatari, kama vile tu kumwona daktari wakati wa uja-uzito kunaweza kuzuia matatizo baadaye. * Hata hivyo, kumbuka kwamba madaktari hawawezi kufanya miujiza. Ponyo kamili la magonjwa yetu yote litatukia tu wakati Mungu atakapofanya “vitu vyote kuwa vipya.”—Ufunuo 21:4, 5.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 8 Ona habari “Mama Wenye Afya, Watoto Wenye Afya,” katika toleo la Amkeni! la Novemba (Mwezi wa 11) 2009.