Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mkia wa Bakteria

Mkia wa Bakteria

 Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mkia wa Bakteria

● Unapoutazama mkia wa bakteria (bacterial flagellum) chini ya darubini yenye nguvu sana, unaonekana kuwa mdogo sana na usio na maana. Umelinganishwa na injini yenye nguvu iliyounganishwa nyuma ya boti. Umefanyizwa jinsi gani?

Kuna aina mbalimbali za mikia, lakini huenda mkia wa bakteria (Kilatini, “mjeledi”) ndio umechunguzwa zaidi. Ukiwa umeunganishwa kwenye ukuta wa chembe ya bakteria, mkia huo huzunguka na kuwezesha bakteria kusonga mbele, kutua, kurudi nyuma, na kugeuka. Inakadiriwa kwamba nusu ya bakteria zote zinazojulikana zina mikia.

Chembe za urithi (DNA) za bakteria au vijidudu zina maagizo kuhusu utendaji wa mkia huo na sehemu ya chembe inayouzungusha. Mkia huo umefanyizwa kwa protini 40, ambazo zinaweza kufananishwa na sehemu za injini. Kwa kustaajabisha, mkia huo hujiunganisha kwa dakika 20 tu!

Kichapo The Evolution Controversy kinasema hivi: “Mkia wa bakteria unatia ndani mtambo wenye kuzunguka ambao huzunguka mara 6,000 hadi 17,000 kwa dakika. Jambo la kushangaza hata zaidi ni kwamba mashini hiyo inaweza kutua na kugeuka haraka, kisha kuzunguka upande ule mwingine mara 17,000 kwa dakika.” Gazeti New Scientist linautaja mkia wa bakteria kuwa “mfano mzuri wa mfumo wenye molekuli tata—mashini ndogo sana ambayo hakuna mhandisi yoyote mwanadamu anayeweza kuiunda.”

Wanasayansi hawajaelewa jinsi ambavyo mkia huo mdogo wa bakteria hujiunganisha pamoja ukifuata mpangilio hususa unaohitajiwa ili sehemu zote 40 zilingane na zifanye kazi vizuri.

Una maoni gani? Je, mkia wa bakteria ulijitokeza wenyewe, au ulibuniwa?

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 24]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Rota

Bushi

Kiunganishi kikuu

Propela

Mikia

[Picha]

Bakteria iliyoongezwa ukubwa

[Hisani]

Bacterium inset: © Scientifica/Visuals Unlimited, Inc.; flagellum diagram: Art source courtesy of www.arn.org