Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mwangaza wa Kimulimuli Usio na Joto

Mwangaza wa Kimulimuli Usio na Joto

 Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mwangaza wa Kimulimuli Usio na Joto

● Katika maeneo ya kitropiki na maeneo yenye joto la wastani, kimulimuli hujulikana kutokana na mwangaza anaotumia kuvutia mwenzi wake. Jambo la kupendeza ni kwamba mwangaza wa kimulimuli ni wenye nguvu kuliko mwangaza wa taa fulani za balbu au zenye mmemeto zilizobuniwa na mwanadamu. Kwa hiyo, utakapotazama gharama yako ya umeme, fikiria kuhusu uwezo wa mdudu huyo mdogo.

Fikiria hili: Taa fulani za balbu za kawaida (incandescent) hutoa asilimia 10 tu ya nishati yote zinazovuta ili kutokeza mwangaza; sehemu ya nishati iliyobaki hugeuzwa kuwa joto na kupotea. Balbu za mmemeto (fluorescent) ni afadhali kwani asilimia 90 ya nishati zinazovuta hutokezwa kama mwangaza. Lakini taa zote mbili hazina uwezo kama wa kimulimuli. Mwangaza huo unaotolewa na kimulimuli huwa na kiasi kidogo cha urujuanimno au infrared, kwa hiyo hawapotezi nishati yoyote wanapotokeza mwangaza!

Kinachomwezesha kimulimuli kufanya hivyo ni utendaji wa kemikali inayoitwa luciferin, kimeng’enya kinachoitwa luciferase na oksijeni. Chembe maalumu zinazoitwa photocytes hutumia luciferase ili kuanzisha utendaji huo kwa kutumia oksijeni kutendesha mchanganyiko huo. Mwishowe zinatokeza mwangaza usio na joto. Sandra Mason, ambaye ni mkufunzi wa ukulima wa bustani na mazingira alisema kuwa huenda mvumbuzi wa balbu za taa Thomas Edison “aliwaonea wivu vimulimuli.”

Una maoni gani? Je, mwangaza wa kimulimuli usio na joto ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 15]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

KIASI CHA MWANGAZA KINACHOTOLEWA

Asilimia 10 Asilimia 90 Asilimia 96

Balbu ya kawaida Balbu ya mmemeto Kimulimuli

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 15]

Firefly on leaf: © E. R. Degginger/Photo Researchers, Inc.; firefly in flight: © Darwin Dale/Photo Researchers, Inc.