Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kombe la Mbawakawa Anayeitwa Cyphochilus

Kombe la Mbawakawa Anayeitwa Cyphochilus

 Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Kombe la Mbawakawa Anayeitwa Cyphochilus

Kombe la mbawakawa anayeitwa Cyphochilus lina magamba membamba sana hata kuliko unywele wa mwanadamu. “Nilipoyachunguza kwa kutumia darubini yenye uwezo mkubwa sana, ni kana kwamba nilikuwa nikiona ulimwengu mwingine,” akasema Dakt. Pete Vukusic wa Chuo Kikuu cha Exeter huko Uingereza. “Lilikuwa jambo lenye kustaajabisha sana.”

Fikiria hili: Vukusic aligundua ni kwa nini mbawakawa huyo ana rangi nyeupe nyangavu. Rangi hiyo inatokana na wembamba wa nyuzinyuzi zinazofanyiza magamba hayo na nafasi zilizo kati ya nyuzi hizo. Umbo hilo hutawanya mwangaza kwa njia inayofaa sana. “Madini fulani yanayotumiwa viwandani kama yale yanayotumiwa kutengeneza aina fulani za karatasi, plastiki, na aina fulani za rangi, yanahitaji kuwa na upana ulio mara mbili zaidi [ya nyuzinyuzi hizo] ili yawe meupe hivyo,” linaripoti gazeti Science Daily.

Wanasayansi wanaamini kwamba kombe la mbawakawa huyo linamsaidia kuchangamana na kuvu weupe mahali anapoishi. Wataalamu wanapendezwa hasa na jinsi rangi ya mbawakawa huyo mdogo inavyoweza kuwafaidi wanadamu, kwa mfano, katika kutengeneza vitambaa vya rangi nyeupe nyangavu vinavyotengenezwa viwandani. Vukusic anasema kwamba vitu kama vile karatasi tunazoandikia, rangi ya meno yetu, na hata kung’aa kwa taa “kutaboreshwa sana ikiwa tekinolojia inaweza kutumia mambo tunayojifunza kutoka kwa mbawakawa huyo.”

Una maoni gani? Je, kombe jeupe la mbawakawa anayeitwa Cyphochilus lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?

[Picha katika ukurasa wa 24]

Mbawakawa anayeitwa “Cyphochilus” ana ukubwa usiozidi ncha ya kidole chako (picha iliyoongezwa ukubwa)

[Hisani]

Department of Entomology, Kasetsart University, Bangkok