Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mabawa ya Viumbe Wanaoruka

Mabawa ya Viumbe Wanaoruka

 Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mabawa ya Viumbe Wanaoruka

▪ Unafikiria ni kitu gani kinachoruka kwa njia nzuri zaidi angani? Je, ni ndege iliyotengenezwa na wanadamu au ni viumbe kama vile popo, wadudu, na ndege? Amini usiamini ndege iliyotengenezwa na wanadamu haikaribii uwezo wa ajabu wa viumbe hao wadogo ambao wana “uwezo wenye kutokeza wa kubaki angani licha ya upepo mkali, mvua, na theluji,” anasema Wei Shyy, profesa wa uhandisi wa vyombo vya angani wa Chuo Kikuu cha Michigan. * Siri yao ni nini? Wanaweza kupiga mabawa yao, jambo ambalo watengenezaji wa ndege wametamani kufanya tangu mwanadamu aanze kutengeneza ndege.

Fikiria hili: Ndege na wadudu fulani wanapokuwa angani, mabawa yao hubadili umbo mara kwa mara ili wakabiliane na mabadiliko ya mazingira. Hilo huwawezesha kukaa angani bila kusonga na kugeuka haraka. Gazeti Science News linaripoti jambo ambalo limeonekana kumhusu popo: “Alipokuwa akiruka kwa mwendo wa polepole, mita 1.5 hivi kwa sekunde, popo alielekeza miisho ya mabawa yake chini na mara moja akaisogeza nyuma alipotaka kwenda juu. Wanasayansi wamegundua kwamba mbinu hiyo . . . inampa nguvu za kusonga mbele.”

Kwa kweli, bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu viumbe wanaoruka. “Wao wanafanyia hewa nini ili kuruka kwa njia nzuri hivyo?” anauliza Peter Ifju, profesa wa ufundi na uhandisi wa vyombo vya angani wa Chuo Kikuu cha Florida. Anaongeza hivi: “Kuna mambo mengi tusiyoelewa juu ya jinsi hewa inavyomzunguka kiumbe anayeruka na jinsi umbo la kiumbe huyo linavyomsaidia kusonga mbele. Tunaweza kuona mambo ambayo [ndege na wadudu] wanafanya, lakini hatuelewi jinsi hilo linavyohusiana na hewa.”

Una maoni gani? Je, bawa linalonyumbulika la viumbe wanaoruka lilijitokeza lenyewe? Au je, lilibuniwa?

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 3 Ingawa viumbe wengi wenye mabawa wanaweza kuruka katika mvua, wengi hutafuta mahali pa kujikinga.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Ndege mvumaji mwenye mdomo mpana

[Hisani]

Laurie Excell/Fogstock/ age fotostock

[Picha katika ukurasa wa 24]

Popo aliye na masikio kama ya panya

[Hisani]

© Delpho, M/age fotostock