Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mguu wa Korongo

Mguu wa Korongo

 Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mguu wa Korongo

▪Korongo hagandi hata akiwa amesimama miguu mitupu juu ya barafu. Kiumbe huyo hudumishaje kiwango cha joto mwilini? Njia moja ni kupitia mfumo wa kudumisha joto.

Fikiria hili: Mfumo huo wa kudumisha joto una mrija ulio na umajimaji wenye joto ulio karibu na mrija mwingine ulio na umajimaji wenye baridi. Umajimaji kwenye mirija hiyo ukielekea upande mmoja ni nusu ya kiwango cha joto kitakachopitishwa. Lakini umajimaji ukielekea pande tofauti kiwango chote cha joto kitapitishwa.

Mfumo huo wa kudumisha joto unapunguza kiwango cha joto cha damu inayoelekea miguuni hadi karibu igande na kisha huipasha joto damu hiyo inaporudi. Mtaalamu wa ndege, Gary Ritchison, anaandika hivi kuhusu ndege wanaoishi katika maeneo yenye baridi: “Mfumo huo wa kudumisha joto hufanya kazi vizuri sana hivi kwamba wanadamu wameuiga katika ujenzi ili kuzuia kupoteza nishati.”

Una maoni gani? Je, mfumo wa kudumisha joto katika miguu ya korongo ulijitokeza wenyewe? Au je, ulibuniwa? *

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 6 Mfumo wa kudumisha joto unapatikana pia katika wanadamu, aina fulani za samaki, na wanyama wengine wengi.

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 25]

 

Mfumo wa kudumisha joto katika miguu ya korongo hupasha joto damu inaporudi

[Mchoro]

Nyuzi 32 Selsiasi

Nyuzi 0-5 Selsiasi

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Seagull: © Michael S. Nolan/age fotostock