Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ungejibuje?

Ungejibuje?

Ungejibuje?

NI NANI ALIYESEMA MANENO HAYA?

Chora mstari kuunganisha maneno na mtu aliyeyasema.

Daudi

Yesu

Sulemani

Paulo

1. “Kumwogopa Yehova ndio mwanzo wa hekima.”

2. “Kama vile mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni wao vivyo hivyo.”

3. “Upendo haushindwi kamwe.”

4. “Yehova ni Mchungaji wangu. Sitakosa chochote.”

▪ Zungumzeni Pamoja: Ni jambo gani lingine unalojua kuhusu watu hao wanaotajwa katika Biblia?

ILITUKIA LINI?

Taja majina ya waandikaji wa kila moja ya vitabu vya Biblia vilivyoonyeshwa hapo chini, na uchore mstari kuunganisha kitabu na mwaka unaokadiriwa kuwa kilikamilishwa kuandikwa.

1450 K.W.K. 1090 K.W.K. 1078 K.W.K. 36 W.K. 56 W.K.

5. Yoshua

6. Ruthu

7. Waroma

MIMI NI NANI?

8. Nilitabiri kwamba Sisera atauawa na mwanamke.

MIMI NI NANI?

9. Mimi na mume wangu tulihatarisha shingo zetu kwa ajili ya Paulo.

KATIKA TOLEO HILI

Jibu maswali haya na utaje mistari ya Biblia ambayo haijaonyeshwa.

Ukurasa wa 6 Ili kuwa mfuasi wa Yesu, mtu anahitaji kufanya nini? (Luka 9:____)

Ukurasa wa 7-8 Mtume Paulo alisema kutaniko la Kikristo lingepatwa na nini baada ya yeye kuondoka? (Matendo 20:____)

Ukurasa wa 13 Shetani amezifanya nini akili za watu wengi? (2 Wakorintho 4:____)

Ukurasa wa 28 Biblia inasema nini kuhusu ngono kati ya watu wa jinsia moja? (Waroma 1:____)

Watoto Watafute Picha

Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Eleza kwa maneno yako mwenyewe jambo linalotendeka katika kila picha.

(Majibu kwenye ukurasa wa 20)

MAJIBU YA UKURASA WA 31

1. Sulemani.—Methali 9:10.

2. Yesu.—Luka 6:31.

3. Paulo.—1 Wakorintho 13:8.

4. Daudi.—Zaburi 23:1.

5. Yoshua, 1450 K.W.K.

6. Samweli, 1090 K.W.K.

7. Paulo, 56 W.K.

8. Debora.—Waamuzi 4:4, 9.

9. Priska, au Prisila.—Waroma 16:3, 4.