Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Makanisa Yanaelekea Wapi?

Makanisa Yanaelekea Wapi?

Makanisa Yanaelekea Wapi?

MAKANISA yanayodai kuwa ya Kikristo yanapatwa na nini? Mahali unapoishi, je, idadi ya watu wanaoenda kanisani inapungua au inaongezeka? Mara kwa mara utasikia madai ya kwamba watu wameanza tena kupendezwa na dini, na ripoti za makanisa kufurika watu huko Afrika, Ulaya Mashariki na Marekani. Hata hivyo, ripoti kutoka sehemu nyingine za ulimwengu, hasa Ulaya Magharibi, zinaonyesha kwamba makanisa yanafungwa, idadi ya watu wanaoenda kanisani inapungua, na watu wengi hawapendezwi na dini.

Kwa sababu ya kupungua kwa wahudhuriaji, makanisa mengi yamebadilisha mitindo yao. Mengine yanadai “hayamhukumu” mtu yeyote na hivyo kuonyesha kwamba Mungu hukubali mwenendo wowote. Isitoshe, badala ya kufundisha Neno la Mungu, makanisa mengi yanaandaa burudani na vivutio vingine visivyohusiana na dini. Ingawa waumini fulani wanaona mabadiliko hayo kuwa yanafaa katika ulimwengu huu wa kisasa, watu wengi wanyofu wanajiuliza ikiwa makanisa yanakengeuka kutoka kwenye utume ambao Yesu aliyapa. Acheni tuchunguze mwelekeo ambao makanisa yamechukua katika miaka ya karibuni.