Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Jamii za Wanyama Zinazokabili Hatari ya Kutoweka

Jamii za Wanyama Zinazokabili Hatari ya Kutoweka

Jamii za Wanyama Zinazokabili Hatari ya Kutoweka

Na mwandishi wa Amkeni! nchini Italia

Orodha ya Mimea na Wanyama Waliomo Hatarini iliyotolewa na Shirika la Kuhifadhi Viumbe Ulimwenguni (IUCN), ambalo makao yake makuu yako Gland, Uswisi, huonyesha hali ya afya ya mimea na wanyama ulimwenguni. Orodha ya Mimea na Wanyama Waliomo Hatarini ya 2004 ina zaidi ya jamii 15,500.

Mojawapo ya visababishi vikubwa vinavyohatarisha jamii hizo ni wanadamu. Badala ya kutunza mazingira, ambayo ni muhimu kwa uhai wake, mwanadamu anaendelea kuyaharibu kwa kufanya mambo yanayohatarisha sana jamii nyingine. Kwa kusikitisha, hilo limefanya jamii nyingi na maliasili zenye thamani zipotee.

Mnyama mmoja aliyekuwa kwenye orodha ya mwaka uliopita ni pomboo wa kawaida mwenye mdomo mfupi, aliye kwenye picha. Zaidi ya asilimia 50 ya idadi yao imepungua katika Bahari ya Mediterania katika kipindi cha miaka 30 hadi 45 iliyopita, na sasa anasemekana kuwa yumo hatarini. Kulingana na IUCN, sababu zinazochangia upungufu huo ni “kupungua kwa chakula cha pomboo katika Mediterania kwa sababu ya mabadiliko ya mazingira, kuvua samaki kupita kiasi, na kuharibiwa kwa mazingira.” Inaonekana pia kwamba viwango vya juu vya kemikali zenye kudhuru zinazotokezwa na mwanadamu na ambazo zilipatikana katika pomboo wa Mediterania “zinaweza kupunguza uwezo wa mfumo wao wa kinga na kuwafanya wasiweze kuzaa.”

Muumba hatawavumilia milele watu waharibifu, wasiojali, na wenye ubinafsi. Tofauti na hilo, unabii wa Biblia unaonyesha kwamba “wakati uliowekwa” unakaribia ambapo ‘atawaharibu wale wanaoiharibu dunia.’ Wakati huo, Yehova Mungu atarudisha hali ambapo wanadamu watatunza ifaavyo “kila kiumbe hai” na ‘mimea yote iliyo juu ya uso wa dunia.’—Ufunuo 11:18; Mwanzo 1:28-30.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Pomboo wa kawaida wenye mdomo mfupi

[Hisani]

© Goran Ehlme/SeaPics.com

[Picha katika ukurasa wa 18]

Alibatrosi huyu yuko pia kwenye orodha ya walio hatarini