Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ni Sinema Gani Zitakazoonyeshwa Msimu Huu?

Ni Sinema Gani Zitakazoonyeshwa Msimu Huu?

 Ni Sinema Gani Zitakazoonyeshwa Msimu Huu?

WEWE hupenda kufanya nini wakati wa likizo? Ikiwa kutakuwa na joto huenda ukafurahia kuwa nje, labda kwenda ufuoni au kwenye bustani.

Hata hivyo, nchini Marekani, watengenezaji wa filamu wanatazamia mamilioni ya watu watumie saa nyingi za msimu huo wakiwa ndani ya majumba ya sinema. Kuna majumba ya sinema zaidi ya 35,000 nchini Marekani peke yake, na katika miaka ya karibuni asilimia 40 hivi ya mapato yanayotokana na kuuzwa kwa tiketi za sinema hupatikana katika msimu wa kiangazi. * Heidi Parker wa gazeti la Movieline anasema hivi: “Faida inayopatikana hulingana na ile ambayo wafanyabiashara hupata wakati wa Krismasi.”

Mambo hayakuwa hivyo sikuzote. Msimu wa kiangazi haukuleta faida kwa majumba ya sinema huko Marekani, hivyo mengi yalipunguza ratiba yao au mengine yalifungwa msimu huo. Lakini kufikia miaka ya katikati ya 1970, majumba mengi ya sinema yenye vifaa vya kupunguza joto yaliwavutia watu wengi kwani nje kulikuwa na joto jingi. Pia watoto walikuwa wamefunga shule na kwa kuwa hawakuwa na kitu kingine cha kufanya, watengenezaji wa sinema walihakikisha kwamba wamewanasa. Muda si muda, msimu wa kiangazi ukawa wakati wa kuonyeshwa kwa sinema iliyopata mafanikio makubwa. Jambo hilo lilibadili jinsi ambavyo filamu hutengenezwa na kuuzwa, kama tutakavyoona.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 3 Nchini Marekani, msimu wa kiangazi wa kuonyesha sinema huanza mwezi wa Mei na kuendelea hadi mwezi wa Septemba.