Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Ijapokuwa Yuda alikusudia kuwaandikia ndugu zake Wakristo kuhusu wokovu ambao walikuwa nao kwa pamoja, aliona ni muhimu awaandikie kuhusu nini? (Yuda 3)

2. Yesu Kristo aliyejivika mwili wa kibinadamu alijiunga na Kleopa na mwenzake walipokuwa wakisafiri kuelekea kijiji gani? (Luka 24:13-32)

3. Kulingana na simulizi la Biblia, ni nini kilichotumiwa kuandika zile Amri Kumi kwenye mabamba mawili ya mawe? (Kutoka 31:18)

4. Wale “wake wengi wageni” wa Sulemani ‘waliogeuza moyo wake ukafuata miungu mingine,’ walikuwa wa mataifa gani? (1 Wafalme 11:1, 4)

5. Ijapokuwa Yesu alifanya miujiza mingi, ndugu zake walishindwa kufanya nini? (Yohana 7:5)

6. Ingawa katika pindi mbili tofauti wana wawili wa Mfalme Daudi, yaani, Absalomu na Adoniya, walijaribu kunyakua ufalme, ni yupi aliyekuwa karibu kufanikiwa? (2 Samweli 16:15-22; 1 Wafalme 1:9-11, 38-53)

7. Mawe ya mvua ya ufananisho yaliyoanguka wakati malaika wa saba alipomwaga bakuli yake ya hasira ya Mungu yalikuwa na uzito gani? (Ufunuo 16:21)

8. Biblia huwataka washiriki wa kutaniko la Kikristo watendeje wakati mmoja wao anapotengwa na ushirika? (1 Wakorintho 5:11)

9. Katika njozi, Ezekieli aliona wanawake Waebrania walioasi imani wakimlilia mungu gani wa uongo? (Ezekieli 8:14)

10. Kwa nini Aguri, ambaye aliandika sura ya 30 ya kitabu cha Methali, aliomba asipewe “umaskini wala utajiri?” (Methali 30:8, 9)

11. Hezekia alipewa ishara gani ili kumhakikishia kwamba Yehova atamponya na kwamba atalinda Yerusalemu dhidi ya Waashuri? (Isaya 38:5-8)

12. Msamaria mwema alimfanyia nini yule mtu aliyekuwa amepigwa na kuachwa karibu kufa kwenye barabara ya kuelekea Yeriko? (Luka 10:34)

13. Kuhani mkuu wa Israeli alipaswa kuvalia nini kichwani? (Kutoka 28:37)

14. Kwa nini Abrahamu alidai mara mbili kwamba Sara alikuwa dada yake? (Mwanzo 12:19; 20:2)

15. Baraka za kutii Sheria ya Mungu na laana za kuivunja, zingetangazwa katika milima gani miwili? (Kumbukumbu la Torati 11:29)

16. Sauli, ambaye alikuwa mfalme wa kwanza wa Israeli, alitoka katika jiji gani? (1 Samweli 10:24-26)

17. Mfalme aliyemtupa Danieli kwenye shimo la simba aliitwa nani? (Danieli 6:9, 16)

Majibu ya Maswali

1. Aliwaandikia ili ‘kuwahimiza wafanye pigano kali kwa ajili ya imani’

2. Emau

3. Kwa “kidole cha Mungu”

4. Walikuwa “Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti”

5. ‘Kumwamini’

6. Absalomu

7. Talanta moja (karibu kilo 20)

8. Kuacha kuchangamana katika ushirika pamoja na mtu huyo

9. Tamuzi

10. Ili asije akashiba na kumkana Yehova au kuiba na kulishambulia jina la Mungu

11. Jua lilirudi nyuma vipandio kumi juu ya vipandio vya ngazi ya Ahazi

12. Aliyafunga majeraha yake, kisha akampeleka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza

13. Kilemba

14. Kwa kuwa Sara alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri, Abrahamu alihofia kwamba Farao na Mfalme Abimeleki wangemuua ili wamuoe Sara

15. Baraka katika Mlima Gerizimu; Laana katika Mlima Ebali

16. Gibea

17. Dario