Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mazingira Ule mfululizo “Je Tunaweza Kuokoa Mazingira?” ulinipendeza sana. (Novemba 22, 2003) Ninatarajia kwa hamu wakati ambapo Yehova ataisafisha dunia yake maridadi na kuirudisha katika hali yake ya awali. Mimi huhuzunika sana kuona jinsi ambavyo mwanadamu ameiharibu dunia yetu!

D. L., Uingereza

Nina umri wa miaka 15, nami sikuwa nikisoma matoleo fulani ya Amkeni! Lakini baada ya kusoma mfululizo huu, nimeazimia kuyasoma kwa ukawaida! Makala hizo zilinifundisha mambo mengi yenye kupendeza kuhusu dunia. Baadaye nilitumia habari hii shuleni na kupata maksi za juu.

S. V., Ukrainia

Ugonjwa wa Mfumo wa Neva Tafadhali pokeeni shukrani zangu za kutoka moyoni kwa ajili ya ile makala “Kuishi na Ugonjwa wa Mfumo wa Neva.” (Novemba 22, 2003) Mwaka mmoja hivi umepita tangu ilipogunduliwa kwamba nina ugonjwa huo. Siwezi tena kutumia mikono, miguu, na jicho langu la kushoto. Hapo awali nilikuwa na maoni yasiyofaa. Lakini kama ilivyopendekezwa katika makala yenu, ninajitahidi kucheka na kuwa na maoni yanayofaa. Asanteni sana kwa makala yenu yenye kutia moyo.

M. A., Japani

Nimekuwa na ugonjwa huu kwa miaka 14. Lakini haujulikani sana huku Japani. Hivyo nilipojua kwamba makala hii inatayarishwa, nilimweleza mume wangu na marafiki zangu kutanikoni. Sasa wananijali sana na kunisaidia.

N. S., Japani

Makala hii inaeleza ugonjwa huo, jinsi unavyozidi, na athari zake kwa usahihi kabisa! Maswali ambayo nimejiuliza kwa miaka mingi yamejibiwa hatimaye. Marafiki wangu wengi wa karibu wameniambia kwamba hawakujua jinsi mtu anavyohisi anapokuwa na ugonjwa huo.

M. W., Ujerumani

Mimi ni mama ya watoto watatu na sina mume. Nilisoma makala hiyo nilipokuwa hospitalini baada ya kupata ugonjwa huo mara ya nne. Makala hiyo ilinigusa moyo sana. Ijapokuwa ni jambo la kushangaza, ugonjwa huo usioweza kutibiwa umeimarisha sana uhusiano wangu pamoja na Yehova na kunifanya nimtumaini zaidi.

M. H., Ujerumani

Makala hii itatusaidia sisi tulio na ugonjwa wa mfumo wa neva. Ingawa sasa ninatumia kiti cha magurudumu, mimi ni mhubiri wa wakati wote, na ninahubiri hasa kwa simu nikiwa nyumbani. Kwa kuwa nimepooza, dada mmoja Mkristo aliandika barua hii kwa niaba yangu.

M. G., Ufaransa

Iligunduliwa kuwa nina ugonjwa wa mfumo wa neva miaka 21 hivi iliyopita. Mimi ni mzee Mkristo, lakini ndugu wamerahisisha kazi yangu ili ugonjwa wangu usizidi. Huo utakuwa wakati mzuri kama nini ambapo “hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa,’” kama vile andiko la Isaya 33:24 linavyosema!

E. C., Marekani

Msiba Huko Mississippi Nilishangazwa sana na makala “Mto Ulipogeuza Mkondo.” (Novemba 22, 2003) Ilinionyesha jinsi ambavyo kuna nguvu nyingi za asili na kwamba mwanadamu hawezi kufanya lolote anapokabili msiba. Makala yenu imeimarisha azimio langu la kuitumaini Biblia.

M. J., Mauritania

Ingawa mambo yaliyosimuliwa yalitukia karibu miaka 200 iliyopita, nilihisi ni kana kwamba yalikuwa yakisimuliwa na mtu aliyeyaona kwa macho. Nilipokuwa nikisoma makala hiyo nilihisi kana kwamba nilikuwa hapo nikipambana na maji yenye nguvu. Nilisoma kila fungu kwa hamu.

V. R., Urusi