Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Samweli alikuwa nabii katika kipindi cha kuhani mkuu yupi? (1 Samweli 3:10-13)

2. Waamori waliuitaje Mlima Hermoni? (Kumbukumbu la Torati 3:9)

3. Mke wa pili wa Abrahamu alikuwa nani, na alipata wana wangapi? (Mwanzo 25:1, 2)

4. Kwa nini divai mpya haiwekwi katika viriba vilivyozeeka? (Luka 5:37)

5. Upanga ambao Ehudi alitumia kumwua Mfalme Egloni wa Moabu mwenye uonevu ulienda wapi? (Waamuzi 3:16-22)

6. Kwa nini Yesu anaitwa “Wakili Mkuu wa Uzima”? (Matendo 3:15; 4:12)

7. Kwa nini ni Yehova pekee anayeweza kutajwa kuwa mkamilifu kabisa? (2 Samweli 22:31; Marko 10:18)

8. Kuhusu dhabihu za wanyama, kwa nini “mafuta yote ni ya Yehova”? (Mambo ya Walawi 3:9-16)

9. Ni ndege gani mwindaji mwenye nguvu anayejulikana kwa uwezo wake wa kuona mbali? (Ayubu 39:27, 29)

10. Ni jina gani la cheo linalotumiwa katika Biblia kumrejelea Yehova, wengine wanaoabudiwa, na wanadamu? (Kutoka 7:1)

11. Yehova alimtumia nabii gani kutabiri jinsi ambavyo ufalme wa Sulemani ungegawanywa? (1 Wafalme 11:29-32)

12. Alipotoa mfano kuhusu jinsi alivyotamani kuwakusanya watu wa Yerusalemu wasiotii, Yesu alimtaja ndege yupi wa kufugwa? (Luka 13:34)

13. Yesu alisema “taa ya mwili” ni nini? (Mathayo 6:22)

14. Danieli alihakikishiwa kwamba unabii wake ungeeleweka wakati gani? (Danieli 12:4)

15. Paulo aliwatorokaje Wayahudi waliopanga njama ya kumwua huko Damasko? (Matendo 9:25)

16. Ni nini ‘kimewapotosha watu kutoka kwenye imani’ na kuwaletea “maumivu mengi”? (1 Timotheo 6:10)

17. Kwa kufuata mwongozo wa Yehova, Musa aliwatuma wapelelezi wangapi Kanaani, na ni nani waliotoa ripoti njema? (Hesabu 13:2; 14:6-9)

18. Kaisari anayetajwa kwenye Matendo 25:11, ambaye Paulo alikata rufani kwake wakati wa kesi yake mbele ya Festo, alikuwa nani?

Majibu ya Maswali

1. Eli

2. Seniri

3. Ketura; sita

4. Kwa sababu divai inapochachuka, itapasua ngozi isiyonyumbulika ya viriba hivyo

5. Egloni alikuwa mnene sana hivi kwamba upanga wote uliingia tumboni

6. Kwa kuwa “hakuna wokovu katika mwingine yeyote.” Fidia ilitolewa kupitia Yesu na yeye ndiye Hakimu aliyewekwa rasmi

7. Ni Yehova tu asiye na mipaka, ukuu wake hauwezi kulinganishwa na yeyote, anastahili sifa zote, naye ni mkuu katika sifa na nguvu zake

8. Kwa kuwa mafuta yalionwa kuwa sehemu yenye thamani zaidi ya mnyama, hilo lilionyesha kwamba sehemu iliyo bora zaidi ni ya Yehova

9. Tai

10. Mungu

11. Ahiya

12. Kuku

13. Jicho

14. “Wakati wa mwisho”

15. Wakati wa usiku wanafunzi wake walimshusha katika kapu kupitia shimo ukutani

16. “Kupenda pesa”

17. Kumi na wawili; Yoshua na Kalebu

18. Nero