Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mitindo Ningependa kutoa shukrani zangu kwa ajili ya ule mfululizo wa makala zenye kichwa, “Je, Wewe Ni Mtumwa wa Mitindo?” (Septemba 8, 2003) Nikiwa kijana, nimehisi nikikazwa na ulimwengu ninunue mavazi ya mtindo wa karibuni zaidi na kuwa na umbo “bora.” Lakini makala hizo zimenisaidia kubadili jinsi ninavyotumia pesa na kuvaa kwa kiasi.

M. B., Marekani

Nina umri wa miaka kumi. Mwalimu wetu alituambia tufanye utafiti kuhusu mitindo. Nilileta nakala ya ile makala yenye kichwa, “Madhara ya Sura Yenye Kuvutia.” Mwalimu wetu alitoa nakala kwa ajili ya wanafunzi wote darasani!

G., Ubelgiji

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 19. Mimi huona ni vigumu kuepuka kutamani kuwa mwanamke mwenye umbo “bora.” Sina umbo kama la wanamitindo, na mara nyingi hilo hunifanya nihisi kwamba sipendezi. Mara kwa mara mimi hutaka kubadili mazoea yangu ya kula ili nipunguze uzito. Punde baada ya kusali nipate ushauri utakaoniwezesha kukabiliana na hisia hizo, nilipokea gazeti hilo, nalo lilikuwa na jibu la sala yangu. Asanteni sana.

S., Ujerumani

Makala hizo zilinisaidia kuelewa ubatili wa kutaka kufuatia mitindo. Nina umri wa miaka 14. Nchini Italia, si rahisi kwenda shuleni ikiwa huna mavazi yenye jina la mbuni au kampuni maarufu kwani utaonwa kuwa duni! Makala zenu zilinifundisha kwamba jambo la maana ni kuwa tajiri kiroho machoni pa Mungu.

F. G., Italia

Okidi Nilifurahia sana kusoma ile makala yenye kichwa “Fahari ya Okidi.” (Septemba 8, 2003) Nilipata madokezo kuhusu kukuza okidi nyumbani na kujifunza baadhi ya majina yake na vyanzo vyake. Gazeti la Amkeni! lilinipa habari nilizokuwa nikitafuta.

L.E.C., Bangladesh

Meno Safi Sina budi kuwaandikia kuhusu ile makala yenye kichwa, “Kijiti cha Kusugua Meno.” (Septemba 8, 2003) Sikuzote nilitaka kujua jinsi watu walivyokuwa wakisafisha meno yao kabla dawa ya meno haijavumbuliwa. Kwa hiyo nilistaajabishwa sana na makala hiyo!

D. G., Marekani

Sikuzote nilikuwa nikipuuza tabia ya kutafuna vijiti. Lakini nilikuwa nikikosea. Inaonekana kwamba kutafuna vijiti kuna manufaa, na sasa mimi mwenyewe nitatumia kimoja ili kulinda meno yangu.

A. A., Chad

Insha Kuhusu Maangamizi Ile makala yenye kichwa “Insha Yake Ilivutia Kwelikweli” ilisema kwamba Wayahudi walikuwa wakivalia Nyota ya Daudi katika kambi za mateso (Septemba 8, 2003). Hata hivyo, kulingana na mambo niliyojionea mimi mwenyewe katika kambi ya mateso ya Ravensbrück, Wayahudi hawakuvalia Nyota ya Daudi bali pembetatu ya manjano.

J. R., Afrika Kusini

“Amkeni!” linajibu: Inaonekana kwamba Nyota ya Daudi haikuvaliwa na Wayahudi katika kambi nyingi. Hata hivyo, kuna uthibitisho kwamba ilivaliwa katika kambi fulani.

Dhuluma Mimi si Shahidi wa Yehova. Hata hivyo, ule mfululizo wa makala zenye kichwa, “Utafanyaje Ukidhulumiwa?” (Agosti 22, 2003) ulitokea kwa wakati unaofaa kabisa. Binti yangu amekuwa akidhulumiwa sana na wanafunzi wenzake shuleni. Kama mlivyopendekeza, nilizungumza naye, nikamtegemeza na kumsaidia. Asanteni kwa kuwajali watu.

T. M., Ukrainia