Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kudhulumiwa Jana usiku binti yangu mwenye umri wa miaka saba alisema kwamba hataki kurudi shuleni kwa sababu ya wasichana wawili waliokuwa wakimdhulumu nyakati zote. Nilianza kusoma mfululizo wa makala wenye kichwa “Utafanyaje Ukidhulumiwa?” (Agosti 22, 2003) Nimetumia makala hizi kumsaidia binti yangu na pia zimenisaidia kujua kinachowafanya watu watende kwa njia fulani.

L. H., Marekani

Nilikuwa nikitukanwa, nikiaibishwa mbele ya wafanyakazi wenzangu na kupuuzwa na mmoja wa wasimamizi wangu mpaka nikaacha kazi. Jambo hilo limeniathiri sana mpaka sasa. Hata hivyo, baada ya kusoma makala hizo, ninahisi vizuri, nikijua kwamba kuna mtu anayeelewa hali yangu.

H. N., Japani

Makala hizo zilinikumbusha jinsi maisha yangu yalivyokuwa. Nilipokuwa mwanafunzi, nilidhulumiwa kila siku. Sikujua ni kwa nini. Makala hizo zilinisaidia kuelewa sababu na zilinifariji.

M. M., Japani

Nilipokuwa shuleni nilipuuzwa na watu na jambo hilo lilinifanya nisijiamini. Nilifundishwa kwamba ninapaswa kucheka ninapodhulumiwa, lakini mlisema kweli kwamba ni afadhali kuwatazama wale wanaokudhulumu uso kwa uso na kuwaeleza kwa utulivu kwamba hufurahishwi na matendo yao.

M. G., Ufaransa

Nakubali kwamba haikuwa rahisi kusoma makala hizo kuhusu dhuluma kwa sababu nilidhulumiwa kimwili, kwa maneno, na kwa njia zisizo za moja kwa moja nilipokuwa kijana na nikiwa mtu mzima. Baada ya kusoma makala hizo, sasa ninaelewa ni kwa nini nimekuwa na maoni mabaya na kujidharau. Kwa hiyo ninataka kuwashukuru kwa makala hizo zilizotoa ushauri mzuri wenye kufariji.

A. M., Italia

Tangu nilipojiunga na shule ya sekondari, nimekuwa nikidhulumiwa kila siku. Makala hizo zimenisaidia kujua kwamba sipaswi kujiona sifai kwa kuwa niko katika dini ndogo. Kadiri wakati unavyopita, ninazidi kujivunia kuwa Shahidi wa Yehova, na ninafurahi iwapo nitateswa kwa sababu hiyo. Nilikuwa nikikasirika. Sasa ninajua la kufanya na nina hakika mambo yatakuwa mazuri.

M. S., Italia

Mimi na dada yangu pacha tuna umri wa miaka 16 na tuko katika darasa moja. Wanafunzi wenzetu wanajua kwamba sisi ni Mashahidi wa Yehova, nao hutudhulumu mara nyingi. Habari hizo kuhusu dhuluma zilielezwa kwa njia halisi na hilo lilitutia moyo sana.

E. P., Italia

Nilibubujikwa na machozi niliposoma makala hizo kwa kuwa nilikumbuka mambo yote ambayo wanafunzi wenzangu walinitendea kila siku kwa miaka sita. Nikiwa kijana, nilifikiri ni mimi tu niliyedhulumiwa. Hata sikujua kwamba mambo hayo niliyopitia yanaitwa dhuluma. Sasa nikiwa mwanamke kijana, ninashukuru sana kufahamu tatizo hilo. Hatimaye ninahisi kwamba watu wananielewa!

A. P., Ujerumani

Nimedhulumiwa sana shuleni hivi kwamba wakati mwingine sitaki kwenda huko. Hata hivyo, makala hizo zimenisaidia kuchanganua hali yangu, nazo zilitoa ushauri mzuri. Ninatumia baadhi ya madokezo yaliyotolewa na yamenisaidia. Asanteni kwa makala hizo zenye kutia moyo na zenye kusaidia.

M. T., Urusi