Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Yesu alimwambia mtu aliyekuwa kipofu aende akanawe wapi ili aweze kuona? (Yohana 9:7)

2. Yesu alikuwa wapi aliposhawishiwa na Shetani ajirushe ili malaika wamwokoe? (Mathayo 4:5, 6)

3. Kwa nini watu wengi sana walimsihi Yesu “ili wapate kuugusa tu upindo wa vazi lake la nje”? (Mathayo 14:35, 36)

4. Ni kitu gani kilichotumiwa nyakati za kale kufulia mavazi na pia kupunguza chuma kama vile risasi na fedha? (Isaya 1:25)

5. Mzaliwa wa kwanza wa Rebeka aliitwa nani, na kwa nini? (Mwanzo 25:25, 30)

6. Yehova aliweka matakwa gani ya kuwachagua wapelelezi 12 waliotumwa kwenye nchi ya Kanaani? (Hesabu 13:2)

7. Paulo aliandika barua yake kwa Waebrania akiwa katika nchi gani? (Waebrania 13:24)

8. Sulemani alikamilisha ujenzi wa hekalu katika mwezi gani wa Kiyahudi? (1 Wafalme 6:38)

9. Ni wanaume gani wawili waliotegemeza mikono ya Musa mpaka Yehova alipowapa Waisraeli ushindi dhidi ya Waamaleki? (Kutoka 17:12)

10. Ni mdudu gani anayejulikana kwa bidii yake na hekima ya kisilika? (Methali 6:6)

11. Badala ya kwenda Ninawi kama vile Yehova alivyokuwa amemwagiza, Yona alijaribu kutorokea wapi? (Yona 1:2, 3)

12. Musa aliijenga wapi ile maskani? (1 Mambo ya Nyakati 21:29)

13. Kwa kuwa Walawi hawakuwa wamegawiwa eneo, walikuwa wanategemezwaje? (Hesabu 18:21)

14. Yesu alimtokea Kleopa na mwanafunzi mwenzake wapi katika siku aliyofufuliwa? (Luka 24:13)

15. Yehova aliwateua nani wawe wasanii wakuu wa kujenga maskani? (Kutoka 31:1-11)

16. Paulo alitumia usemi gani kuwaita wale waliofanya kazi pamoja naye? (Wafilipi 4:3)

17. Kwa nini Yehova aliwaamuru Waisraeli waweke uzi wa bluu juu ya upindo kwenye miisho ya nguo zao? (Hesabu 15:37-40)

18. Ni mbao za aina gani zilizofanyiza wale makerubi wawili na milango ya Patakatifu Zaidi? (1 Wafalme 6:23, 31)

19. Kama alivyoandika Zekaria, Yehova alitumia maneno gani kuonyesha jinsi Anavyohisi watu wake wakionewa? (Zekaria 2:8)

20. Baba ya Yezebeli alikuwa nani? (1 Wafalme 16:31)

21. Kwa nini Pilato alijaribu kumwachilia Yesu? (Luka 23:4)

Majibu ya Maswali

1. Dimbwi la Siloamu

2. Ukuta wa mnara wa hekalu

3. Walitaka kuponywa magonjwa yao

4. Sabuni (yenye sodiamu kaboneti au potasiamu kaboneti)

5. “Esau” kwa sababu alizaliwa akiwa na nywele nyingi na “Edomu” kwa sababu aliku- bali kubadilisha haki yake ya uzawa kwa mchuzi mweku- ndu wa denge

6. “Mtu mmoja kwa ajili ya kila kabila la baba yake, kila mmoja wao mkuu kati yao”

7. Italia

8. Buli, mwezi wa nane wa kalenda takatifu

9. Haruni na Huru

10. Chungu

11. Tarshishi

12. Nyikani

13. Makabila yale mengine yaliwapa sehemu ya kumi ya kila zao na mifugo

14. Kwenye barabara inayokwenda Emau

15. Bezaleli na Oholiabu

16. “Wafanyakazi wenzangu”

17. Ili kuwakumbusha kwamba walikuwa watu watakatifu kwa Yehova na wanapaswa kuzishika amri zake

18. Mbao za mfuta

19. “Yeye anayewagusa ninyi anaigusa mboni ya jicho langu”

20. Ethbaali, mfalme wa Wasidoni

21. Hakuona uhalifu kwake