Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Wanadamu Waiga Usanii wa Muumba

Wanadamu Waiga Usanii wa Muumba

Wanadamu Waiga Usanii wa Muumba

Kwa nini balbu za umeme hazivunjiki zinapowekwa kwenye vishikilio vyake? Kitabu How in the World? kinasema hazivunjiki kwa sababu zimetengenezwa kwa kuiga “umbo la yai.” Ingawa ganda la yai ni jembamba sana, yai halivunjiki wakati kuku anapolilalia. Hiyo ni kwa sababu ya umbo la yai ambalo hulifanya lihimili uzito wa kuku. (Kama lingekuwa nene vifaranga hawangeweza kulivunja na kutoka.) Kwa kuiga usanii wa Muumba, balbu zina umbo la duara na hivyo zinaposhikwa kwa nguvu, nguvu hizo “husambaa pande zote kwa sababu ya umbo lake.” Kwa hiyo, kama yai, balbu haziwezi kuvunjika kwa sababu nguvu nyingi hazilemei sehemu moja. Mwanadamu amejifunza mengi kutokana na uumbaji!