Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Yehova Ndiye Hunifariji”

“Yehova Ndiye Hunifariji”

“Yehova Ndiye Hunifariji”

MANENO yaliyo juu ni tafsiri ya shime rasmi ya Mfalme Charles wa Tisa wa Sweden. Shime hiyo inasema hivi katika Kilatini: “Iehovah solatium meum.” Mfalme huyo alikuwa mmoja wa wafalme katika nasaba ya wafalme wa Sweden waliotawala kuanzia mwaka wa 1560 hadi 1697. Wafalme hao walitumia jina la Mungu katika Kiebrania na Kilatini kwenye sarafu, nishani, au kwenye shime zao. Charles wa Tisa pia alianzisha Chama cha Kifalme cha Yehova. Alipotawazwa katika mwaka wa 1607, Charles alivalia mkufu ulioitwa mkufu wa Yehova.

Kwa nini wafalme hao walikuwa na mazoea hayo? Wasomi wanaamini kwamba walichochewa na wanaharakati Wakalvini wa Ulaya na heshima yao kwa Biblia. Kwa kuwa walikuwa wafalme wenye elimu wakati wa kipindi cha Mvuvumko, inaonekana walifahamu jina la Mungu, Yehova, katika Kilatini. Bila shaka wengine walijua jina hilo lilipatikana mara elfu nyingi katika maandishi ya awali ya Biblia ya Kiebrania.

Imethibitika wazi kuwa katika sehemu fulani za Ulaya katika karne za 16 na 17, jina Yehova liliandikwa kwenye sarafu na nishani na vilevile kwenye majengo ya umma na makanisa. Huenda maneno yanayopatikana kwenye Zaburi 83:18 yalikubaliwa na kuheshimiwa na wengi: “Wajue ya kuwa wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.”

[Picha katika ukurasa wa 31]

MKUFU NA BEJI YA CHAMA CHA KIFALME CHA YEHOVA, mwaka wa 1606, ulioundwa kwa dhahabu, enameli, kwazi ya fuwele, na vito vyekundu

MFALME ERIK WA KUMI NA NNE 1560-1568

MFALME CHARLES WA TISA 1599-1611 (ndugu ya Erik wa Kumi na Nne)

MFALME GUSTAVUS WA PILI ADOLPH 1611-1632 (mwana wa Charles wa Tisa)

MALKIA CHRISTINA 1644-1654 (binti ya Gustavus wa Pili Adolph)

[Hisani]

Chain: Livrustkammaren, Stockholm Sverige; coins: Kungl. Myntkabinettet, Sveriges Ekonomiska Museum