Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 24. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Kwa nini mhubiri alisema kwamba “kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi”? (Mhubiri 4:12)

2. Chini ya Sheria ya Musa, mnyama aliyefaa kuliwa alipaswa kuwa na sifa gani mbili? (Kumbukumbu la Torati 14:6)

3. Baba ya Yoshua aliitwa nani? (Yoshua 1:1)

4. Shetani alifanya nini aliporuhusiwa na Yehova kumdhuru Ayubu? (Ayubu 2:7)

5. Ni nani aliyemwambia Mfalme Ahasuero kuhusu mti wa mikono 50 ambao Hamani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Mordekai, na hivyo kumfanya mfalme aamuru kwamba Hamani atundikwe juu yake? (Esta 7:9)

6. Yesu alisema manabii wasio wa kweli wangetambuliwaje? (Mathayo 7:15, 16)

7. Ni jina lipi la cheo la Yehova linalopatikana tu katika kitabu cha Danieli ambalo linakazia daraka lake akiwa Hakimu mkubwa zaidi na mwenye kuheshimiwa zaidi? (Danieli 7:22)

8. Ni bidhaa gani zenye thamani ambazo zililetwa na merikebu za Mfalme Solomoni za Tarshishi kila baada ya miaka mitatu? (1 Wafalme 10:22)

9. Ni nani aliyemsaidia Aroni kuitegemeza mikono ya Musa iliyoinuliwa mpaka Yehova akawapa Waisraeli ushindi dhidi ya Waamaleki? (Kutoka 17:12)

10. Wanafunzi walitumia njia gani kuamua yule ambaye angechukua mahali pa Yudasi Iskariote? (Matendo 1:23-26)

11. Ni nani aliyekuwa kuhani wa cheo cha juu wa Israeli wakati Samweli alipokuwa nabii? (1 Samweli 3:1)

12. Wakati wa kuweka wakfu ukuhani katika Israeli, Musa alitia damu kwenye sehemu zipi tatu za Aroni na wanawe? (Mambo ya Walawi 8:23, 24)

13. Mungu alitumia nini kumuumba Hawa, badala ya kumuumba kutokana na udongo? (Mwanzo 2:21, 22)

14. Paulo alisema “mzizi wa mambo mabaya ya namna zote” ni nini? (1 Timotheo 6:10)

Majibu kwa Maswali

1. Ili kukazia kwamba wale wanaofanya kazi kwa umoja wakiwa na lengo moja wana nguvu na uwezo zaidi wa kupambana na matatizo

2. Alipaswa kuwa mnyama anayepasua kwato na kucheua

3. Nuni

4. ‘Alimpiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa’

5. Harbona, mmojawapo wa wasimamizi-wa-nyumba

6. “Kwa matunda yao”

7. ‘Mzee wa Siku’

8. Dhahabu, fedha, pembe, nyani, na tausi

9. Huri

10. Walisali na kupiga kura

11. Eli

12. Sikio la kuume, kidole gumba cha mkono wa kuume na cha mguu wa kuume

13. Ubavu uliotoka kwa Adamu

14. “Kupenda fedha”