Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Coelacanth—samaki Asiyepatikana kwa Urahisi

Coelacanth—samaki Asiyepatikana kwa Urahisi

Coelacanth—samaki Asiyepatikana kwa Urahisi

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI KENYA

MNAMO Aprili 2001, samaki wa kike aina ya coelacanth alivuliwa karibu na pwani ya Kenya. Samaki huyo alikuwa na urefu wa meta 1.7 na uzani wa kilogramu 77. Kwa kawaida samaki huyo huwa na mkia wenye sehemu tatu, rangi ya bluu na madoadoa meupe.

Wakati fulani, ilidhaniwa kwamba samaki huyo alikuwa amekwisha toweka kabisa. Kisha, mnamo mwaka wa 1938, samaki huyo alivuliwa karibu na pwani ya Afrika Kusini. Uvumbuzi huo ulikuwa mojawapo ya mavumbuzi ya wanyama yenye kustaajabisha zaidi katika karne ya 20. Kabla ya hapo, samaki huyo alitajwa tu kwenye rekodi za visukuku. Tangu samaki huyo alipovuliwa kwa mara ya kwanza, samaki wengine wa aina yake wameonekana karibu na Msumbiji na Madagaska. Samaki wengi wa aina hiyo wamepatikana pia kwenye Visiwa vya Komoro.

Mayai ya samaki wa kike aina ya coelacanth hayaanguliwi ndani ya maji. Badala yake, samaki hao hutaga mayai mwilini mwao na kuyaangua humohumo au mara tu yanapotoka mwilini. Mayai 17 yalitolewa ndani ya mwili wa yule samaki wa kike aliyevuliwa mwaka jana. Kila yai lilikuwa kubwa kama mpira wa tenisi.

Viumbe wa baharini kama vile samaki aina ya coelacanth huonyesha ule unamna-namna wa uumbaji na kutukuza hekima ya Muumba wao, Yehova Mungu.—Zaburi 148:7.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 23]

Picha na michoro: Ichthyology Department/NATIONAL MUSEUMS OF KENYA