Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mtetezi wa Vita Au Mteteaji wa Amani?

Mtetezi wa Vita Au Mteteaji wa Amani?

Mtetezi wa Vita Au Mteteaji wa Amani?

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI SWEDEN

Kila mwaka, watu au mashirika ambayo yamejitahidi sana kuboresha hali za wanadamu katika fani mbalimbali hupewa tuzo ya Nobeli. Zoea hilo lilianza lini, na linahusianaje na jitihada za kupata amani ya ulimwenguni pote?

ANAJULIKANA kwa kuchangia maendeleo ya wanadamu. Hata hivyo, alitajirika sana kwa kuuza silaha za vita. Ni nani huyo? Ni Alfred Bernhard Nobel, mwenyeji wa Sweden aliyekuwa mtaalamu wa kemia ambaye alimiliki viwanda. Nobel amesifiwa kwa matendo yake ya fadhili, lakini pia ameitwa “mwuzaji wa kifo.” Kwa nini? Kwa sababu Nobel alibuni baruti kali na alitajirika sana kwa kuunda na kuuza makombora hatari.

Hata hivyo, uvumbuzi fulani wenye kustaajabisha ulifanywa baada ya kifo cha Nobel mnamo mwaka wa 1896. Wasia wake ulisema kwamba dola milioni 9 za Marekani zitengwe na kwamba kila mwaka watu wanaopata mafanikio makubwa ya fizikia, kemia, tiba, fasihi, na amani wapewe riba inayotokana na fedha hizo.

Hapo mwanzoni, watu wengi walishangaa. Inawezekanaje mwuzaji wa makombora kutaka sana kuwakabidhi tuzo watu waliofanya matendo ya fadhili na hata ya kuleta amani? Wengine walidhani kwamba Nobel alisumbuliwa na dhamiri yake kwa sababu alikuwa ametengeneza silaha hatari. Hata hivyo, wengine waliamini kwamba Nobel alikuwa akijitahidi kuleta amani. Yaonekana aliamini kwamba silaha zikiwa hatari zaidi, vita haingetokea. Inaripotiwa kwamba alimwambia hivi mwandishi mmoja: “Huenda viwanda vyangu vitakomesha vita haraka kuliko mabaraza yenu.” Kisha akaongeza hivi: “Wakati ambapo vikosi viwili vya jeshi vitaangamizana mara moja, huenda mataifa yote yaliyostaarabika yataogopa na kuvunja majeshi yao.”

Je, maneno ya Nobel yalitimia? Ni masomo gani ambayo watu walijifunza katika karne iliyofuata kifo cha Nobel?

[Blabu katika ukurasa wa 3]

“Ninataka kubuni kifaa au mashine itakayoweza kuharibu vitu vingi sana hivi kwamba vita itakoma kabisa”—ALFRED BERNHARD NOBEL

[Picha katika ukurasa wa 3 zimeandaliwa na]

Ukurasa wa 2: Kombora: U.S. Navy photo; vifusi vya jengo: UN PHOTO 158178/J. Isaac; ukurasa wa 3: Nobel: © Nobelstiftelsen