Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Wanyama Wasiojulikana wa Vietnam

Wanyama Wasiojulikana wa Vietnam

 Wanyama Wasiojulikana wa Vietnam

“KILIKUWA kipindi chenye kusisimua cha uvumbuzi wa wanyama katika karne hii,” akasema Douglas Richardson, mtunza-mamalia katika Bustani ya Wanyama ya London. Alikuwa anarejezea uvumbuzi wa aina fulani ya wanyama wakubwa katika misitu nchini Vietnam katika miaka kumi iliyopita.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walishindwa kufika katika misitu hii kwa sababu ya vita vikali. Hata hivyo, sasa watafiti wa wanyama wanaofanya kazi huko, wamefaulu kuwapiga picha wanyama wanaopatikana katika misitu hii kwa kutumia kamera za pekee. Miongoni mwao ni kifaru wa Vietnam wa jamii ya Javan. Vifaru hao ni mojawapo ya wanyama walio hatarini.

Baadhi ya wanyama wasiojulikana wa Vietnam ni ng’ombe dume anayefanana na paa anayejulikana pia kama Vu Quang . Mnyama huyu aliyevumbuliwa mwaka wa 1992 katika hifadhi ya wanyama ya Vu Quang, ana uzito wa kilogramu 100 na urefu wa meta moja kufikia mabegani. Labda ni wa jamii ya ng’ombe, paa au mbuzi. Katika hifadhi hiyohiyo, mbawala watatu waligunduliwa —mbawala mkubwa sana aitwaye muntjac aligunduliwa mwaka wa 1993, Truong Son muntjac mwaka wa 1997, na leaf muntjac mwaka wa 1998.

Katika mwaka wa 1996, wanasayansi kwenye Uwanda wa Tainguen huko Vietnam, waligundua mnyama mdogo mla-nyama anayependa kutembea usiku, aitwaye Ngawa wa Tainguen. Ana uzani wa kati ya kilogramu 3 hadi 7.5 naye huishi katika misitu ya kitropiki yenye unyevunyevu.

Richardson alieleza kwamba wanyama wadogo wanaendelea kupatikana—hata jamii tofautitofauti zipatazo 20 za vyura wa kitropiki hupatikana kila mwaka—lakini kupatikana kwa wanyama wakubwa ni jambo ambalo halikutarajiwa, laripoti gazeti The Independent la London.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Ngawa wa Tainguen

Ng’ombe dume aina ya “Vu Quang”

“Truong Son muntjac”

Kifaru wa Vietnam

[Hisani]

Msitu: © Wildside Photography

Kifaru wa Vietnam: AP Photo/World Wildlife Fund, Mike Baltzer; wanyama wengine watatu: Courtesy EC-SFNC/Acknowledging the European Commission’s support of the photo-trapping program