Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 21. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Kulingana na Petro, mtu apaswa kuonyesha sifa gani ili apokee fadhili isiyostahiliwa ya Mungu? (1 Petro 5:5)

2. Baada ya utawala wa siku saba wa Zimri, mfalme wa tano wa Israeli, ni wanaume gani wawili waliopigania ufalme wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka minne? (1 Wafalme 16:21)

3. Ni nini kilichowatia hofu Waisraeli hivi kwamba wakakataa kuingia Bara Lililoahidiwa? (Hesabu 13:28, 31-33, BHN; Kumbukumbu la Torati 1:28)

4. Ni nini kipimo kikubwa zaidi cha uzito na cha thamani ya pesa kwa Waebrania? (Ezra 8:26)

5. Feliksi alimwita Paulo kwa kisingizio gani, lakini nia yake hasa ilikuwa nini? (Matendo 24:24-26)

6. Ni usemi gani ambao Yesu alitumia kujirejezea na kuwarejezea wanafunzi wake? (Mathayo 5:14; Yohana 8:12)

7. Ni jina gani linalotumika tu kwa Yesu wala si kwa wafuasi wake? (Mathayo 23:10)

8. Yakobo alitumia usemi gani kurejezea tamaa ya makuu, umaarufu, na mamlaka? (Yakobo 4:1)

9. Ni kifaa kipi cha ujenzi kilichotumiwa sana katika jumba la kifalme la Uajemi kule Shushani? (Esta 1:6)

10. Kulingana na Yohana, ni vitu gani vitatu vya ulimwengu ‘visivyotokana na Baba’? (1 Yohana 2:16)

11. Katika orodha ya Paulo ya silaha za kiroho za Mkristo, ni sehemu gani inayofananisha wokovu? (Waefeso 6:17)

12. Ni nani aliyewaheshimu wanawe zaidi ya Yehova? (1 Samweli 2:27-29)

13. Herufi ya tano ya alfabeti ya Kiebrania ni gani? (Zaburi 111:3, NW)

14. Solomoni alianza ujenzi wa hekalu katika mwezi gani wa kalenda ya Kiyahudi? (1 Wafalme 6:1)

15. Ni nabii yupi Mkristo aliyetabiri kwamba Paulo angekamatwa huko Yerusalemu? (Matendo 21:10, 11)

Majibu ya Maswali

1. “Hali ya akili ya kujishusha chini,” au unyenyekevu

2. Tibni na Omri

3. Wenyeji walikuwa “wakubwa sana” na wenye nguvu sana

4. Talanta

5. Ili kusikiliza juu ya “itikadi katika Kristo Yesu”; hongo

6. “Nuru ya ulimwengu”

7. Kiongozi

8. “Kufurahisha hisi za mwili”

9. Marimari

10. “Tamaa ya mwili,” “tamaa ya macho,” na “wonyesho wa mtu wa kujivunia njia yake ya kutegemeza maisha”

11. Kofia ya chuma

12. Eli, Kuhani wa Cheo cha Juu

13. He

14. Zivu

15. Agabo