Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ukosefu wa Kazi ya Kuajiriwa Ninataka kuwaambia jinsi nilivyotiwa moyo niliposoma makala “‘Kazi ya Kudumu’ Imepatwa na Nini?” (Oktoba 8, 2000) Madokezo ya jinsi ya kujitayarisha kwa uwezekano wa kupoteza kazi na jinsi ya kupambana na tatizo la ukosefu wa kazi ya kuajiriwa yalikuwa mazuri sana. Sasa siogopi sana mahojiano ya kazi ninayotazamia.

F. W., Marekani

Duka la Dawa za Kichina Nina wasiwasi kuhusu dhana ya tiba ya badala inayoelezwa katika makala “Kuzuru Duka la Dawa za Kichina.” (Novemba 8, 2000) Sisemi matibabu ya mitishamba ni mabaya. Hata hivyo, je, yin na yang huwakilisha tu joto na baridi? Mlionyesha tu sehemu ndogo ya maana ya fundisho ambalo lina msingi katika uchawi na dini isiyo ya kweli. Je, hiyo si hatari?

V. A., Marekani

Ni kweli kwamba kanuni ya “yin” na “yang” imetumiwa katika maeneo mengi huko Mashariki, kutia ndani uaguzi. Hata hivyo, jambo hilo halifanyi iwe vibaya kuitumia kwa njia inayokubalika katika Maandiko, kama vile kutambua magonjwa. Kwa hiyo, ni lazima kila Mkristo aamue binafsi ikiwa anataka kukubali matibabu yanayotegemea kanuni hiyo.—Mhariri.

Matatizo ya Watoto Niliguswa sana na mfululizo wa “Matatizo ya Watoto—Suluhisho Hatimaye!” (Desemba 8, 2000) Kumbukumbu zangu za utotoni ni zenye kuhuzunisha. Mama yangu alikuwa mlevi na alinitenda vibaya karibu kila siku. Muda si muda nilishuka moyo na mara nyingi nilitaka kufa. Mfululizo huo ulinikumbusha jinsi uhusiano kati ya wazazi na watoto ulivyo muhimu sana. Kwa kuwa sasa nimejua kwamba Yehova ananipenda, ninajaribu kumwelewa mama yangu, yeye vilevile alitendwa vibaya utotoni.

U. P., Jamhuri ya Korea

Mimi ni mwalimu, mwenyeji wa Argentina, na ninaona kwamba ingekuwa jambo zuri sana ikiwa wazazi wote na walimu wote wangefuata ushauri wa mfululizo huo—na ushauri wa Biblia, ambayo mnainukuu mara nyingi.

F. S., Hispania

Hasira Nilisoma sehemu yenye kichwa “Hasira na Moyo Wako” katika “Kuutazama Ulimwengu.” (Desemba 8, 2000) Ni kweli kabisa. Nina ugonjwa wa moyo ambao hufanya nichoke na kusikia vibaya mara nyingi. Siwezi kujiruhusu kukasirika nikiwa shuleni ingawa hilo ni jambo gumu sana. Hata hivyo, Yehova Mungu amenisaidia kuondoa hasira maishani mwangu.

A. F., Marekani

Matatizo ya Tezi-Kibofu Nilithamini sana makala iliyotoka hivi majuzi ya “Kukabiliana na Matatizo ya Tezi-Kibofu.” (Desemba 8, 2000) Hata hivyo, haikutaja matibabu ya kuingiza mbegu iliyonururishwa. Hivi majuzi matibabu hayo yametangazwa katika magazeti ya Marekani nayo yana athari chache tu za baadaye.

H. Z., Marekani

Asante kwa kuwajulisha wasomaji wetu juu ya matibabu hayo. Ripoti zinaonyesha kwamba matibabu ya kuingiza mbegu iliyonururishwa (“brachytherapy”) yanaweza kuwa na matokeo mazuri kama vile upasuaji wa kawaida na yasiyo na athari nyingi. Hata hivyo, madaktari hawajajua bado matokeo yake ya kudumu. Kwa sasa, wagonjwa wapaswa kujulishwa matibabu yote kabla ya kuchagua matibabu.—Mhariri.

Yellowstone Ninawapongeza kwa makala ya “Yellowstone—Chimbuko la Maji, Mwamba, na Moto”! (Desemba 8, 2000) Mimi na mke wangu tulifurahia kufanya kazi katika hifadhi hiyo mwaka uliopita. Mke wangu alifanya utafiti kwa kutumia kompyuta, na mimi nilichunguza mabwawa. Kwa hiyo, tulipoipokea makala hiyo, tulisisimuka na tukaisoma mara moja. Vema! Mlichagua picha zinazofaa, na utafiti ulikuwa bora. Habari zote zilikuwa sahihi. Lakini ili kuelewa kabisa fahari ya hifadhi hiyo, lazima mtu aione na macho! Ni maridadi sana.

D. S., Marekani