Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ulimwengu Nilifurahia sana ule mfululizo wenye kichwa “Ulimwengu—Je, Ulitokea kwa Nasibu?” (Oktoba 8, 2000) Lilikuwa jambo la kupendeza kuona jinsi Yehova Mungu aliumba kila kitu kwa utaratibu. Makala hiyo inaonyesha wazi kwamba sisi tuliumbwa wala hatukutokea kupitia mageuzi.

E. V., Marekani

Usalama Unaposafiri kwa Ndege Asanteni sana kwa makala “Kufanya Usafiri wa Ndege Uwe Salama Zaidi.” (Septemba 22, 2000) Hata hivyo, niliona kwamba chumba cha rubani kilichoonyeshwa kwenye picha si cha ndege aina ya Boeing 747 kama ilivyosemwa bali ni cha ndege aina ya Boeing 777.

M. R., Czechia

Hatukuweza kupata picha za chombo cha kuiga hali halisi ya usafiri cha ndege aina ya Boeing 747. Hivyo, makala ilisema kuwa chombo hicho cha kuiga hali halisi ya usafiri cha aina ya 747 ‘kinafanana na kile kimeonyeshwa.’—Mhariri.

Soko la Hisa Asanteni kwa makala yenye usawaziko “Je, Ni Hekima Kutega Uchumi Katika Soko La Hisa?” (Oktoba 8, 2000) Mambo niliojionea maishani yamenifundisha niwe mwangalifu kuhusu habari za hisa zinazotiliwa shaka. Mara nyingi mtu akifuata habari hizo atapata hasara kubwa. Kabla ya kununua hisa, ni jambo la hekima kujua jinsi mambo yalivyo katika soko.

N. B., Ujerumani

Sikubaliani na lile dai kwamba kutega uchumi katika soko la hisa si kumtumainia mungu wa “Bahati.” (Isaya 65:11) Kuweka pesa katika mfumo unaobadilika-badilika haraka na unaofanya kazi bila mpango maalumu, ni kucheza kamari.

P. B., Marekani

Ni kweli kwamba kutega uchumi katika soko la hisa kwaweza kuwa hatari sana. Na kama inavyokuwa katika biashara nyingi, mambo yasiyotazamiwa huwepo. Hata hivyo, si sahihi kusema kwamba biashara ya hisa ni kucheza kamari. Kucheza kamari huhusisha kutoa pesa bila kupata bidhaa zozote. Hata hivyo, hisa huwakilisha kile mtu anachomiliki katika biashara fulani. Basi biashara ya hisa yaweza kuonwa kuwa ununuzi na uuzaji wa bidhaa halali.—Mhariri.

Uhamisho Katika Siberia Niliimarishwa na uaminifu wa Stepan na wa ndugu wengine Wakristo uliotajwa katika simulizi la Alexei Davidjuk, “Hangaiko Langu Kuu—Kudumu Mwaminifu.” (Oktoba 8, 2000) Niliathiriwa na sababu iliyotolewa kuonyesha ni kwa nini ndugu mmoja alikosa uaminifu—“kwa sababu aliacha kusoma na kuamini Biblia.” Maneno hayo yameniimarisha kuendelea kujifunza Maandiko Matakatifu kwa ukawaida.

A. V., Georgia

Michezo Hatari Hivi majuzi nilialikwa kushiriki mchezo wa kuelea angani kwa kutumia ndege inayonyiririka bila kutumia nguvu za injini. Mwaliko huo ulinivutia sana lakini nilitaka kujua maoni ya Biblia juu ya jambo hilo. Siku chache baadaye, nilipokea jibu kupitia makala yenu “‘Michezo Hatari’—Je, Ujihatarishe?” (Oktoba 8, 2000) Bila shaka mchezo huo unaonekana kuwa unapendeza sana. Lakini siwezi kuhatarisha uhai wangu kwa kushiriki mchezo huo kwa kuwa uhusiano wangu na Yehova ni wa maana sana.

M.M.S., Brazili

Mlisema kwamba Shetani alimshawishi Yesu “yamkini katika njozi.” Kwani vishawishi hivyo havikutukia kihalisi?

C.G.H., Marekani

Mambo fulani ya simulizi hilo la Biblia huwa magumu kueleweka yakionwa kihalisi. Kwa mfano, hakuna mlima mrefu sana kiasi cha kwamba Shetani angeweza kumwonyesha Yesu “falme zote za ulimwengu na utukufu wazo.” Wala haiwezekani kuwa Yesu angemruhusu Shetani kihalisi ‘amchukue kwenda pamoja naye kuingia lile jiji takatifu’ au ‘kumsimamisha juu ya buruji ya hekalu.’ (Mathayo 4:5-8) Basi, ni wazi kwamba njozi ya aina fulani ilihusishwa. Haidhuru njia aliyotumia, Shetani alimshawishi Yesu kikweli. Kwa kukataa kushawishwa, Yesu alionyesha uaminifu-maadili wake usioweza kuvunjwa.—Mhariri.