Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Mahakama kuu ya Wayahudi iliitwaje? (Matendo 5:27)

2. Yesu anatimiza kwa mafanikio mambo fulani yanayohusiana na kusudi la Mungu katika kipindi kipi kinachotajwa na mtume Yohana? (Ufunuo 1:10)

3. Goliathi alikuwa na silaha zipi tatu alipomjia Daudi ili kupigana naye? (1 Samweli 17:45)

4. Mke wa Hosea alikuwa nani? (Hosea 1:3)

5. Ni nani waliogundua kwamba Wasiria waliozingira Samaria walikuwa wamekimbia? (2 Wafalme 7:3-5)

6. Ahasuero Mfalme wa Uajemi aliwatolea watu wote katika milki yake nini alipomfanya Esta kuwa malkia wake? (Esta 2:18)

7. Baada ya kumwumba Adamu, ni hali gani ambayo Yehova alisema haikumfaa? (Mwanzo 2:18)

8. Yehova alimwagiza Yoshua afanye nini kuhusiana na farasi wa adui za Waisraeli, na hivyo kuwatia moyo Waisraeli wamtegemee Yehova ili kupata ulinzi? (Yoshua 11:6)

9. Ni nini kinachoweza kuzuia hasira? (Mithali 15:1)

10. Kwa nini kuna maandishi yanayotangulia zaburi nyingi? (Zaburi 3-9)

11. Ayubu alitumia usemi gani alipotaka kuonyesha kwamba alikuwa ameponyoka pasipo kitu chochote? (Ayubu 19:20)

12. Yesu alikuwa nyumbani mwa nani aliposhtakiwa na Mafarisayo na waandishi kwa kula na kunywa pamoja na wakusanya-kodi na watenda-dhambi? (Luka 5:29, 30)

13. Sheria ya Musa ilikataza kula sehemu gani ya mnyama wa dhabihu? (Mambo ya Walawi 7:23-25)

Majibu ya Maswali

1. Sanhedrini

2. “Siku ya Bwana”

3. Upanga, fumo, na mkuki

4. Gomeri

5. Watu wanne wenye ukoma

6. Msamaha

7. ‘Kuwa peke yake’

8. Kutema farasi na kuchoma moto magari

9. Jawabu la upole

10. Ili kutambulisha mwandishi, kuandaa maagizo ya muziki, na maelezo juu ya maana au kusudi la zaburi

11. “Ngozi ya meno yangu”

12. Nyumbani mwa Lawi, au Mathayo

13. Mafuta