Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Historia Je, Tuitumaini?

Historia Je, Tuitumaini?

Historia Je, Tuitumaini?

“Kujua mambo yaliyopita hutufanya . . . tujione tukiwa sehemu ya jamii ambayo imekuwapo kwa miaka mingi kabla hatujazaliwa na itakayokuwapo baada ya kifo chetu.”Kitabu A COMPANION TO THE STUDY OF HISTORY, CHA MICHAEL STANFORD.

KUTOJUA historia ni kutokuwa na kumbukumbu lolote maishani. Pasipo historia ni kana kwamba wewe, familia yako, kabila lako, au hata taifa lako halina asili, wala mwanzo. Matukio ya sasa hayangekuwa na msingi wala maana yoyote pasipo historia.

Historia yaweza kuwa na masomo muhimu sana maishani. Inaweza kutusaidia kuepuka kufanya makosa yaleyale kila mara. Mwanafalsafa mmoja alisema kwamba watu wanaosahau mambo yaliyopita hawana budi kuyarudia. Kufahamu historia kwaweza kutuelimisha kuhusu ustaarabu wa kale, ugunduzi wenye kustaajabisha, watu mashuhuri, na kutusaidia kuona mambo kwa njia mbalimbali.

Lakini kwa kuwa historia ni elimu inayohusiana na watu na matukio ya kale, tutajuaje iwapo inaweza kutumainiwa? Ikiwa tutajifunza masomo muhimu kutokana na historia, basi bila shaka ni sharti masomo hayo yategemee ukweli. Na tunapofahamu ukweli, tunapaswa kuukubali, japo huenda usipendeze nyakati zote. Mambo yaliyopita yanaweza kulinganishwa na bustani ya maua ya waridi—ni maridadi na pia ina miiba; inaweza kupendeza sana, na inaweza pia kudunga.

Katika makala zifuatazo, tutachunguza nyanja mbalimbali za historia ambazo zinaweza kutusaidia kuchanganua usahihi wa yale tunayosoma. Tutachunguza pia jinsi rekodi zenye kutegemeka za historia zinavyoweza kumnufaisha msomaji mwenye utambuzi.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Malkia Nefertiti

[Picha katika ukurasa wa 3]

Twaweza kujifunza masomo gani kutokana na historia?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Nefertiti: Ägyptisches Museum der Staatlichen Museen Preußischer Kulturbesitz, Berlin

Pambizoni: Photograph taken by courtesy of the British Museum