Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kaboni Monoksaidi Mwuaji Asiyeonekana

Kaboni Monoksaidi Mwuaji Asiyeonekana

Kaboni Monoksaidi Mwuaji Asiyeonekana

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI UINGEREZA

TAKRIBAN watu 50 hufa kila mwaka huko Uingereza kutokana na sumu ya kaboni monoksaidi inayotokezwa na vifaa vyenye hitilafu vya kupasha nyumba joto. “Mbali na asbesto, kaboni monoksaidi ndiyo sumu inayoathiri watu wengi sana kazini na nyumbani,” charipoti Kituo cha Hadhari cha London. Kaboni monoksaidi ni nini?

Kaboni monoksaidi ni gesi inayofanyizwa wakati kitu kinaposhindwa kuchomeka kabisa, iwe ndani ya injini ya gari au katika vifaa vinavyopasha nyumba joto vinavyotumia makaa ya mawe au fueli nyingine za visukuku, hasa gesi. Haina rangi yoyote, harufu yoyote, wala ladha yoyote. Inauaje?

Chembe nyekundu za damu hupeleka oksijeni muhimu sana kwenye tishu za mwili. Hatari ya kaboni monoksaidi ni kwamba hiyo hufyonzwa na chembe nyekundu za damu badala ya oksijeni. Sumu ya kaboni monoksaidi huathiri mwili uendeleapo kukosa oksijeni. Kupumua kiasi kidogo cha kaboni monoksaidi kwa muda fulani kwaweza kutokeza madhara ya kudumu kwa ubongo. Dalili za madhara hayo zatia ndani kuumwa na kichwa, kusinzia, udhaifu, kizunguzungu, kichefuchefu, kuzimia—na katika hali mbaya sana, mpigo dhaifu wa moyo, kuzirai, na kushindwa kabisa kupumua. Mtu anapolemewa ghafula na gesi hiyo, anahitaji kupewa oksijeni papo hapo na asaidiwe kupumua kabla ya asphyxiation—uhaba wa oksijeni katika ubongo—kusababisha kifo.

Ni nini kiwezacho kufanywa ili kuzuia hatari za kaboni monoksaidi? Hakikisha kwamba vifaa vyote vya umeme vinawekwa na kukaguliwa kwa ukawaida na mtaalamu. Ikiwa gesi yawaka kwa moto wa manjano badala ya buluu, huko huenda ni kuchomeka kusiko kwa kawaida na yaelekea kunatokeza kaboni monoksaidi. Vifaa mbalimbali vya nyumbani vya kutambua kuwepo kwa kaboni monoksaidi sasa vinapatikana. Tahadhari sikuzote unapotumia vyombo vinavyoweza kutoa kaboni monoksaidi.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Moto usio wa kawaida

[Picha katika ukurasa wa 31]

Moto wa kawaida

[Picha katika ukurasa wa 31]

Vifaa mbalimbali vya nyumbani vya kutambua kuwepo kwa kaboni monoksaidi sasa vinapatikana