Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Yesu alimwambia mwanamke Msamaria Mungu apasa kuabudiwa kwa njia gani? (Yohana 4:24)

2. Ili wavumilie msongo na mnyanyaso, Mungu huwapa nini watumishi wake waaminifu? (2 Wakorintho 4:7-10)

3. Mwana mdogo zaidi wa Mwamuzi Gideoni, mwana pekee kati ya wana 70 aliyekwepa kuuawa na kaka yake wa kambo Abimeleki, alikuwa nani? (Waamuzi 9:5)

4. Mwaka wa 50 baada ya Waisraeli kuingia katika Bara Lililoahidiwa, na uhuru kutangazwa nchini kote uliitwaje? (Mambo ya Walawi 25:10)

5. Watu 12,000 walioajiriwa na wana wa Amoni ili wapigane na Daudi walitoka katika ufalme upi mdogo? (2 Samweli 10:6)

6. Katika mwaka wake wa pili wa utawala, Mfalme Nebukadreza wa Babiloni aliona nini katika ndoto kilichomsumbua sana? (Danieli 2:1, 31)

7. Samsoni alipasua nini mara mbili kwa kutumia mikono yake pekee katika kisa cha kwanza kurekodiwa ambapo alitumia nguvu alizopewa na Mungu? (Waamuzi 14:5, 6)

8. Ni mnyama yupi ambaye Abrahamu alipata amenaswa pembe zake katika kichaka ambaye alimtumia kuwa dhabihu badala ya Isaka? (Mwanzo 22:13)

9. Ni nini alichofanya Mfalme Sauli wakati wa vita dhidi ya Waamaleki na hivyo kuvunja amri ya Yehova? (1 Samweli 15:3-9)

10. Baada ya uhamisho wa Babiloni, mwezi wa kwanza wa Ethanimu katika kalenda ya Kiyahudi, ulipewa jina gani?

11. Wazazi wa Yesu walimpata wapi mwana wao mwenye umri wa miaka 12 baada ya kumtafuta kwa siku tatu? (Luka 2:46)

12. Ni nani aliyeambiwa kwa lugha ya kiunabii afurahi sana kuhusu kuingia kwa Yesu kwa shangwe ya ushindi akiwa juu ya mwana-punda? (Zekaria 9:9)

13. Kwa nini Yesu alitushauri tuweke “hazina mbinguni”? (Mathayo 6:20)

14. Yehova alifanya nini kudhihirisha ghadhabu yake kwa Solomoni, wakati Solomoni alipoanza kutolea dhabihu miungu mingine wakati wa uzeeni? (1 Wafalme 11:14, 23-26)

15. Maandiko hutushauri tulinde nini kuliko yote tuyalindayo? (Mithali 4:23)

16. Mfalme Yehoyakimu alifanya nini aliposomewa hatikunjo zilizokuwa na maagizo ya Yehova dhidi ya Waisraeli? (Yeremia 36:23)

17. Yakobo alidhani mwana wake Yosefu alikuwa ameuawa na nini? (Mwanzo 37:33)

18. Tangu nyakati za kale ni jiji gani lililojulikana kuwa “mji wa mitende”? (Kumbukumbu la Torati 34:3)

Majibu ya Maswali

1. “Roho na kweli”

2. “Nguvu ipitayo iliyo ya kawaida”

3. Yothamu

4. Yubile

5. Ishtobu

6. Sanamu kubwa sana inayofanana na mwanadamu, ambayo sehemu zake zilifanyizwa kwa metali mbalimbali

7. Mwana-simba

8. Kondoo mume

9. Alimwacha hai mfalme wao Agagi, pamoja na mifugo na kundi la wanyama waliokuwa bora

10. Tishri

11. Katika hekalu

12. “Binti Sayuni”

13. Hazina za kimwili huharibika na haziwezi kumletea mtu kibali cha Mungu

14. Alimwondolea baraka zake na akaanza kutokeza wapinzani dhidi ya Solomoni

15. Moyo wa kitamathali

16. Aliikata na kuitupa katika moto

17. “Mnyama mkali”

18. Yeriko