Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Habari za Televisheni—Ni Kiasi Gani Ambacho kwa Kweli Ni Habari?

Habari za Televisheni—Ni Kiasi Gani Ambacho kwa Kweli Ni Habari?

Habari za Televisheni—Ni Kiasi Gani Ambacho kwa Kweli Ni Habari?

Baada ya kuchanganua yaliyomo na yanayotolewa katika habari 102 za televisheni kutoka katika maeneo 52 ya miji mikuu huko Marekani, kikundi cha wachunguzi wa habari kiliona kwamba ni asilimia 41.3 tu ya programu ndiyo iliyokuwa na habari. Ni nini kilicho katika habari hiyo nyingine?

Kwa wastani, asilimia 30.4 ya wakati wa matangazo ya habari za televisheni ni ya kibiashara. Kwa kweli, baadhi ya stesheni zilizochunguzwa zilitumia wakati mwingi zaidi kwa matangazo ya kibiashara kuliko habari. Isitoshe, habari za redioni mara nyingi hujaa mambo yasiyo ya maana, ikasema ripoti iliyokuwa ikifanya muhtasari wa matokeo ya uchunguzi. * Chini ya kichwa “Mambo Yasiyo ya Maana,” ripoti hiyo yaainisha “wakati mwingi wa habari za redioni hutumiwa kwa porojo ya watangazaji, utangazaji, na kuonyeshwa kwa habari zinazokuja, habari ‘zenye kupendeza,’ au habari za kipuuzi na habari zinazohusu watu maarufu.” Mfano wa habari zisizo za maana: “Mashindano ya Sauti Zisizopendeza,” “Ripota Aendesha Kigari ‘kwa Njia ya Kustaajabisha na Isiyo na Kifani,’” na “Watu Wengi Zaidi Wanunua Kipakaza-Sandiwichi Kwenye Maduka Makuu.”

Ni nini ambacho huwa katika habari hasa? Habari za uhalifu zimeenea katika habari za televisheni, zikiwa asilimia 26.9 ya habari za redioni. “‘Habari kuu ni ile ya uuaji,’ ndiyo sera ya wazi katika habari za televisheni . . . Huenda kiwango cha uhalifu kikawa cha chini Marekani kwa miaka michache iliyopita, lakini si katika habari za televisheni.” Kwa nini? Kulingana na waanzilishi wa uchunguzi huo, “matukio ya uhalifu huvutia watu na kunasa uangalifu wao.”

Baada ya uhalifu ni misiba kama vile moto, aksidenti za magari, mafuriko, na milipuko (asilimia 12.2 ya habari), ikifuatiwa na habari za michezo (asilimia 11.4). Kisha mambo ya afya (asilimia 10.1), serikali (asilimia 8.7), na uchumi (asilimia 8.5). Habari kama vile elimu, mazingira, sanaa, na sayansi huwa hazikaziwi uangalifu sana (kuanzia asilimia 1.3 hadi 3.6). Ripoti za hali ya hewa huwa asilimia 10 ya habari zote zinazotolewa. “Kila mtu hupendelea kuzungumza juu ya hali ya hewa na bila shaka habari za televisheni pia,” ndivyo walivyosema wachunguzi. Wanaongeza kusema hivi: “Aina yoyote ya hewa, iwe nzuri au mbaya, joto au baridi, mvua au kavu, yaweza kuvuta uangalifu mwingi wa televisheni.”

Kwa njia yenye kupendeza, ripoti hiyo yasema kwamba idadi inayoongezeka ya waandishi wa habari na watazamaji wanaona uhitaji wa badiliko. Hata hivyo, uchunguzi huo wakubali kwamba badiliko hilo halitakuwa rahisi kwa sababu “uvutano wa kibiashara na pupa vyaweza kutisha ubora wa uandishi wa habari.”

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 3 Ripoti Not in the Public Interest—Local TV News in America ni uchunguzi wa nne wa kitaifa wa kila mwaka wa mambo yaliyo katika habari. Imekusanywa na Dakt. Paul Klite, Dakt. Robert A. Bardwell, na Jason Salzman, wa shirika la Rocky Mountain Media Watch.