Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Hiyo ni Mbinu Mpya!”

“Hiyo ni Mbinu Mpya!”

SOO-JEONG ni mshauri katika shule ya sekondari huko Korea Kusini, hutumia video zilizo katika tovuti ya jw.org kufundishia darasani. Anasema hivi: “Wanafunzi wanafurahia sana kutazama video, Rafiki wa kweli ni nani? Baada ya kuitazama wao husema: ‘Sijawahi fikiria urafiki kwa njia hiyo. Hiyo ni mbinu mpya!’ Baadhi yao waliahidi kutembelea tovuti hiyo wanapohitaji mashauri.” Soo-jeong anaongezea hivi: “Nimewapendekezea wengine watumie video hii wanapofundisha, nao wanafurahia kuitumia.”

Video nyingine ambayo imewasaidia wanafunzi wengi nchini humo ni video ya vibonzo, Mshinde Mnyanyasaji Bila Kutumia Ngumi. Mwalimu fulani anayefanya kazi na Shirika la Kuwalinda Vijana na Jeuri aliwaonyesha wanafunzi wake video hiyo. Alisema hivi: “Wanafunzi wengi huvutiwa sana na video hiyo kwa sababu ina michoro. Kwa kuongezea, video hiyo inafaa kwa sababu inaonyesha njia za kukabiliana na kujilinda na jeuri.” Shirika hilo liliomba kibali cha kutumia video hiyo katika hotuba ambazo hutolewa kwenye shule nyingi za msingi nao walipata kibali. Maofisa wa polisi pia hutumia video zilizo katika tovuti ya jw.org.

Tafadhali tembelea tovuti hiyo. Ni rahisi kuitumia, na unaweza kupakua video, rekodi za kusikiliza, Biblia na machapisho mengine mengi bila malipo yoyote.