ULIMWENGU WENYE MISUKOSUKO
2 | Linda Mapato Yako
KWA NINI NI MUHIMU?
Watu wengi huhangaika kila siku ili kupata mahitaji ya msingi. Kwa kusikitisha, misukosuko ya ulimwengu huu inaweza kufanya hali iwe ngumu zaidi. Kwa nini?
-
Gharama za vyakula na makazi huongezeka sana katika maeneo yenye misukosuko.
-
Majanga yanaweza kusababisha ukosefu wa ajira, au kupungua kwa mishahara.
-
Majanga yanaweza kusababisha uharibifu wa nyumba, biashara, au mali nyingine na kuwalazimisha watu wengi wawe maskini.
Unachopaswa Kujua
-
Kadiri unavyojua kupanga vizuri matumizi ya pesa, ndivyo utakavyoweza kujitayarisha vizuri kwa ajili ya majanga.
-
Kumbuka kwamba unaweza kupoteza kipato, akiba ya pesa, na mali.
-
Kuna vitu ambavyo pesa haiwezi kununua kama vile, furaha na umoja katika familia.
Unachoweza Kufanya Sasa
Biblia inasema hivi: “Tukiwa na chakula na mavazi, tutaridhika na vitu hivyo.”—1 Timotheo 6:8.
Kuridhika kunatia ndani kudhibiti tamaa ya vitu tunavyotaka na kutosheka na mahitaji yetu ya kila siku. Ni muhimu kufanya hivyo hasa ikiwa tumepoteza kazi.
Ili kuridhika, huenda ukahitaji kurekebisha mtindo wako wa maisha. Ukitumia pesa nyingi kuliko kipato chako, huenda hali ikawa mbaya zaidi.