HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ISAYA 34-37
Hezekia Alithawabishwa kwa Sababu ya Imani Yake
Mfalme Senakeribu wa Ashuru alimtuma Rabshake Yerusalemu akawaambie watu wa jiji hilo wasalimu amri. Waashuru walitoa hoja mbalimbali za kuwafanya Wayahudi wasalimu amri bila kupigana.
-
Hakuna atakayewasaidia. Misri haitawasaidia.—Isa 36:6
-
Shaka. Yehova hatawapigania kwa sababu mmemuudhi.—Isa 36:7, 10
-
Vitisho. Hamwezi kulishinda jeshi lenye nguvu la Waashuru.—Isa 36:8, 9
-
Vishawishi. Kujisalimisha kwa Waashuru kutaboresha maisha yenu.—Isa 36:16, 17

