DAFTARI LA MKUTANO WA HUDUMA NA MAISHA

Nehemia Aliipenda Ibada ya Kweli

Kiswahili
Nehemia Aliipenda Ibada ya Kweli
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/202016042/univ/art/202016042_univ_sqr_xl.jpg

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | NEHEMIA 1-4

Nehemia Aliipenda Ibada ya Kweli

Nehemia Aliipenda Ibada ya Kweli

455 K.W.K.

  1. Nisani (Mac./Apr.)

    2:4-6 Nehemia aliomba ruhusa ya kujenga upya Yerusalemu, mahali palipokuwa kitovu cha ibada ya kweli katika siku zake

  2. Iyari

  3. Sivani

  4. Tamuzi (Juni/Jul.)

    2:11-15 Nehemia aliwasili karibu na wakati huu na kuchunguza kuta za jiji

  5. Abi (Jul./Ago.)

    3:1; 4:7-9 Ujenzi ulianza licha ya upinzani

  6. Eluli (Ago./Sept.)

    6:15 Ujenzi wa ukuta ulikamilika baada ya siku 52

  7. Tishri